Halmashauri ya Wilaya ya Newala imenunua lori la tani 18 kwa gharama ya Shilingi milioni 169.9 kupitia mapato yake ya ndani kwa mwaka wa fedha 2024/2025, kwa lengo la kuongeza mapato kupitia shughuli mbalimbali za usafirishaji.
Ununuzi wa lori hili ni mkakati wa halmashauri wa kuongeza mapato kwa kutumia rasilimali zake badala ya kutegemea vyanzo vya nje.
Lori hilo litatumika katika shughuli mbalimbali kama usafirishaji wa taka, vifaa vya ujenzi, na huduma za kukodisha kwa taasisi na wananchi, hatua inayotarajiwa kuongeza mapato ya halmashauri.
Wakazi wa Newala DC,kwa nyakati tofauti wamepongeza hatua hiyo wakisema kuwa itaongeza ajira na kuboresha utoaji wa huduma za kijamii.
Aidha, wameitaka halmashauri kuhakikisha lori hilo linatumika ipasavyo na kutengeneza mpango madhubuti wa usimamizi ili kuhakikisha linazalisha mapato kwa ufanisi na linadumu kwa muda mrefu.
@mtwarars_habari
@ortamisemi
@msemajimkuuwaserikali
@kundya_mwangi
@newalafmtz
@kizurdigital
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa