1. UTANGULIZI
RIdara ya Elimu ya Sekondari ni moja ya idara za Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Idara hii ilianzishwa mwaka 2009 baada ya Serikali kugatua usimamizi na uendeshaji wa shule za sekondari kutoka kwenye Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwenda na kusimamiwa na Mamlaka ya Serikali za Mitaa (Halmashauri za Wilaya/Miji/Manispaa/Majiji). Halmashauri ya wilaya ya Newala ina jumla ya shule 16 zikiwemo 15 za serikali na 1 ya binafsi inayomilikiwa na Mfuko wa Maendeleo wa Wananchi wa Newala. Shule ya Sekondari Mnyambe ya Wavulana yenye kidato cha tano na sita ina Tahasusi za CBG, PCB, HKL na HGK. Shule 15 za serikali zina wanafunzi 5,132 wakiwemo wavulana 2,255 na wasichana 2,877 ambao wanasimamiwa na walimu 171 wakiwemo wanaume 141 na wanawake 30 ambao wanatekeleza majukumu mbali mbali, ambapo walimu 157 wanafundisha katika sekondari 15, walimu 10 ni Maafisa Elimu Kata na 4 wanasaidia utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Halmashauri.
2. DIRA NA MWELEKEO
2.1 DIRA, DHIMA NA MALENGO YA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA 2014
Msingi wa elimu na mafunzo utajikita katika kumjengea Mtanzania misingi bora ya malezi, maadili, ujuzi,umahiri na kumwezesha kujitegemea. Elimu ya kujitegemea itaendelea kuongoza utoaji wa elimu na mafunzo kwa kuzingatia mabadiliko yanayotokea katika jamii, kisiasa, kiuchumi, kisayansi na kiteknolojia.
2.1.1 DIRA
Kuwa na Mtanzania aliyeelimika na mwenye maarifa, stadi, umahiri, uwezo na mitazamo chanya ili kuweza kuchangia katika kuleta maendeleo ya Taifa.
2.1.2 DHIMA
Kuinua ubora wa elimu na mafunzo na kuweka mifumo na taratibu zitakazowezesha kupata idadi kubwa ya Watanzania walioelimika na wanaopenda kujielimisha zaidi ili waweze kuchangia katika kufikia malengo ya maendeleo ya Taifa letu.
2.2 LENGO LA JUMLA LA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO
Kuwa na Watanzania walioelimika na wenye maarifa na ujuzi kuweza kuchangia kwa haraka katika maendeleo ya Taifa na kuhimili ushindani
3. ELIMU YA SEKONDARI
3.1 MATAMKO YA SERA KUHUSU ELIMU YA SEKONDARI
3.1.1 SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 1995
Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 ilifafanua kuwe Elimu ya Sekondari ina maana ya Programu (Mpango) kamili wa elimu inayotolewa kulingana na Mitaala ya Serikali na kupatikana kwa wanafunzi ambao watakuwa wamemaliza elimu ya msingi. Nchini Tanzania elimu rasmi ya shule za Sekondari ina ngazi mbili. Ngazi ya kwanza ni elimu ya sekondari ambayo mwanafunzi husoma kwa muda wa miaka minne, ambapo ngazi ya pili ni Programu ya Miaka miwili ya elimu ya Sekondari (ngazi ya Juu). Ngazi ya kawaida huanzia kidato cha I na kuishia kidato cha 4, wakati Ngazi ya Juu ina kidato cha 5 mpaka cha 6. Hivyo Elimu ya Sekondari itaendelea kuwa ya miaka minne kwa ngazi ya Kawaida na miaka miwili kwa ngazi ya Juu.
3.1.2 MALENGO YA ELIMU YA SEKONDARI (Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 1995).
Elimu ya sekondari nchini inatolewa kwa wanafunzi wahitimu wa elimu ya msingi ambao huchaguliwa baada ya kufikia viwango vinavyotakiwa. Utoaji wa elimu ya sekondari una malengo yafuatayo;
Kuimarisha na kupanua upeo wa msingi wa fikra, maarifa, ujuzi na msingi uliopatikana na kuendelezwa kwenye ngazi ya elimu msingi.
Kuwezesha maendeleo zaidi na kutambua umoja wa Taifa, uraia, na kanuni, kukubalika kibinafsi, kuheshimu kazi na kuwa tayari kufanya kazi, haki za binadamu, maadili ya kiutamaduni na kiroho, mila, tabia na majukumu ya kiraia na masharti yake.
Kukuza maendeleo ya umahiri katika kumudu lugha na matumizi ya kufaa ya ujuzi wa mawasiliano katika Kiswahili na katika angalau lugha moja ya kigeni.
Kutoa fursa ya upatikanaji wa maarifa, ujuzi, mwelekeo na weledi katika maeneo ya kujifunza yanayotakiwa au yaliyochaguliwa.
Kuwaandaa wanafunzi kwa ajili ya elimu ya kati, ya juu, ya ufundi na ufundi stadi.
Kujenga tabia ya uwezo wa kujisomea, kujiamini na kujiendeleza kwenye maeneo mapya ya sayansi na teknolojia, taaluma, maarifa na stadi za kazi.
Kuwaandaa wanafunzi kujiunga na ulimwengu wa kazi.
TAMKO
3.1.2.1 Serikali itaweka utaratibu wa elimu ya awali kuwa ya lazima na kutolewa kwa watoto wenye umri kati ya miaka mitatu hadi mitano kwa kipindi kisichopungua mwaka mmoja.
3.1.2.2 Serikali itaweka utaratibu wa elimumsingi kuwa ya lazima kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha Nne; na kutolewa kwa miaka kumi na umri wa kuanza darasa la Kwanza kuwa kati ya miaka minne hadi sita kulingana na maendeleo na uwezo wa mtoto kumudu masomo katika ngazi husika.
3.1.2.3 Serikali itaweka utaratibu wa kuhakikisha muda wa kukamilisha elimu na mafunzo katika ngazi mbalimbali za elimu baada ya elimumsingi unalenga mwanafunzi kupata ujuzi stahiki kulingana na Mfumo wa Tuzo wa Taifa.
3.1.2.4 Serikali itahakikisha kuwa elimumsingi katika mfumo wa umma inatolewa bila ada.
4. LENGO LA IDARA
Kutoa nafasi ya upataji maarifa, ujuzi na kuelewa ili wanafunzi wajiunge na taasisi za ufundi na mafunzo ya kitaalamu ya elimu ya juu.
5. VITENGO VILIVYOPO KATIKA IDARA
Idara ya elimu ya sekondari ina jumla ya vitengo viwili (2) ambavyo hufanya shughuli zake kwa ushirikiano na kumsaidia mkuu wa idara ambaye ni msimamizi mkuu wa shughuli za idara katika kuleta matokeo tarajiwa.
Vitengo vya idara ni pamoja na a)Kitengo cha Taaluma kinachosimamiwa na Afisa Elimu Taaluma Wilaya
b)Kitengo cha Vifaa na Takwimu kinachosimamiwa na Afisa Elimu Vifaa na Takwimu Wilaya.
Toka kuanzishwa kwa idara ya Elimu Sekondari mwaka 2009, kumekuwa na viongozi mbalimbali toka kuanzishwa kwake hadi sasa kama ifuatavyo:
|
|
|
|
Na.JINA KAMILIJINSICHEOMWAKA KUANZAMWAKA KUMALIZA
1JULIUS K. NESTORYMEDSEO20092012
2OMARY R. KISUDAMEDSAO20092012
3CARITAS MUNYOGWAKEDSEO20122013
4MAGNUS MUNYUKUMESLO2012SASA
5ALICE MSEMWAKEDSEO20132015
6MUSA E. MUSOMAMEDSAO2013SASA
7MAJIDU KALUGENDOMEDSEO20162018
8ABDALAH I. MEMBEMEDSEO20182020
9FRIDAY SONDASYMEDSEO2020SASA
5.1 MAJUKUMU YA IDARA NA VITENGO
Majukumu ya idara ni pamoja na:-
• Kuiwakilisha Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika ngazi zote kuhusu masuala ya elimu ya sekondari.
• Kufafanua na kusimamia utekelezaji wa Sera za Elimu na Mafunzo kwa kufuata miongozo na taratibu, sheria na kanuni zinazoongoza utoaji wa elimu ya sekondari, katika shule za serikali na zisizo na serikali
• Kusimamia masuala yahusuyo maendeleo ya taaluma na michezo katika shule za sekondari wilayani.
• Kuwa mshauri wa masuala ya elimu sekondari katika Wilaya.
• Kusimamia upanuzi wa elimu ya sekondari.
• Kushughulikia masuala ya mitihani ya ndani na nje katika usimamizi na uratibu.
• Kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mipango ya elimu ya sekondari
• Kusimamia na kuratibu masuala yanayohusu kuinua ubora wa mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
• Kudhibiti na kusimamia nidhamu ya walimu na wanafunzi wa shule za sekondari katika Halmashauri.
• Kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa Shule na kufuatilia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa shule za sekondari zilizokaguliwa na uthibiti ubora wa Shule.
• Kupanga walimu wa sekondari kulingana na mahitaji ya kila shule wilayani
• Kusimamia haki na maslahi ya walimu na wanafunzi wa sekondari.
• Kukusanya, kuchambua na kuunganisha takwimu mbalimbali zinazohusu elimu ya sekondari.
• Kufanya ufuatiliaji na Tathmini ya utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo
5.1.1 MAJUKUMU YA AFISA ELIMU TAALUMA (W)
Kuratibu na kusimamia mitihani ya Kitaifa inayoendeshwa kwa shule za sekondari katika Halmashauri.
Kubuni mipango ya mitihani ya elimu ya sekondari na kusimamia utekelezaji wake.
Kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa shule.
Kushughulikia ujazaji wa OPRAS kwa walimu na watumishi wengine wa shule za sekondari.
Kuhakikisha walimu wa shule za sekondari wanapangwa katika shule kwa kuzingatia ikama inayokubalika.
Kubuni na kuratibu mipango ya mafunzokazini kwa walimu na watumishi wengine wa shule za sekondari.
Kusimamia maendeleo ya taaluma na michezo ya shule za sekondari katika Halmashauri.
5.1.2 MAJUKUMU YA AFISA ELIMU VIFAA NA TAKWIMU (W)
Kukusanya takwimu za shule na kuingiza kwenye mfumo.
Kutunza takwimu zote za shule katika Halmashauri.
Kuandaa taarifa za ujenzi wa shule.
Kuingiza bajeti ya idara na shule za sekondari kwenye mfumo wa PLANREP/
Kuwasilisha takwimu za shule katika ngazi ya Mkoa au OR – TAMISEMI zinapohitajika.
Kukusanya takwimu za elimumsingi bila malipo.
6. MUUNDO WA IDARA
Idara imeundwa na ngazi tano. Ngazi ya Wilaya kuna mkuu wa idara ambaye ni Afisa Elimu Sekondari Wilaya. Idarani kuna maafisa wa vitengo viwili ambavyo ni:- Afisa Elimu Taaluma (W) na Afisa Elimu Vifaa na Takwimu (W). Ngazi ya kata wapo Waratibu Elimu Kata wakifuatiwa na Wakuu wa shule pamoja na walimu na watumishi wao katika ngazi ya Shule.
Shule za sekondari zinaendeshwa na Bodi za shule ambazo ni vyombo vya juu vya maamuzi katika shule. Bodi ya shule ni chombo cha kuendesha shule na ndio msemaji mkuu wa masuala ya uendeshaji wa shule. Ni chombo chenye nguvu ya kisheria.
Uongozi wa shule una muundo ufuatao:
7. MIONGOZO NA SERA ZINAZOTUMIWA NA IDARA Katika kutekeleza shughuli zake, idara inatumia Sera na Miongozo mbalimbali inayotolewa na serikali katika kusimamia utoaji wa elimu. Sera na miongozo hiyo ni kama ifuatavyo:-
1. Sera za Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995.
2. Sheria ya Elimu ya mwaka 1978 na marekebisho yake.
3. Miongozo mbalimbali ya elimu
4. Nyaraka mbalimbali za elimu
5. Maagizo mbalimbali ya Serikali
8. HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA IDARA MARA KWA MARA
Nia kuu ya idara ya elimu ya sekondari ni kutoa huduma kwa walimu, wanafunzi na wananchi kwa ujumla kuhusu masuala ya elimu ya sekondari, huduma hizo ni kama ifutavyo;-
• Kusimamia utoaji wa elimu ya sekondari shuleni(Kufuatilia Ufundishaji na ujifunzaji).
• Kutoa ushauri wa kitaalamu wa elimu ya sekondari katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji na maeneo mengine.
• Ufuatiliaji wa miradi ya ujenzi shuleni.
• Kuwahudumia wananchi, wazazi, walezi, walimu na wanafunzi katika masuala yahusuyo elimu ya sekondari.
9. TAARIFA ZA WATUMISHI
Halmashauri ya Wilaya ya Newala kupitia Idara ya Elimu Sekondari ina jumla ya walimu 171 wakiwemo wanaume 141 na wanawake 30 ambao wanatekeleza majukumu mbali mbali, ambapo walimu 157 wanafundisha katika sekondari 15, walimu 10 ni Maafisa Elimu Kata na 4 wanasaidia utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Halmashauri.
Idara ina watumishi watano (4) ambapo kati yao wasio walimu ni mmoja (1) ambaye ni katibu Mahsusi.
JEDWALI NAMBA 1. WATUMISHI WA IDARA YA ELIMU SEKONDARI NA NAMBA ZAO ZA SIMU
NAJINA KAMILIJINSICHEONAMBA ZA SIMU
1FRIDAY SONDASY MWAKASALAMEKAIMU AFISAELIMU SEKONDARI (W)0689533445
2MUSA ERNEST MUSOMAMEAFISAELIMU TAALUMA SEKONDARI (W)0688406880
3MAGNUS MUNYUKU MAGNUSMEAFISAELIMU VIFAA NA TAKWIMU (W)0713849250
4DYNESS PAUL CHILUMBAKEKATIBU MAHSUSI0787075986
JEDWALI NAMBA 2. MAAFISA ELIMU KATA NA NAMBA ZAO ZA SIMU
NA.JINA KAMILIJINSIKATANAMBA ZA SIMU
1ALLY S. NAYOMOMECHIWONGA0674458630
2SUITBERT K. NAMPWAPWAMEMTUNGURU0683079228
3RAPHAEL SIJAONAMEMKWEDU0713082753
4NICHOLAUS F. MILANZIMEKITANGARI0654294566
5JILE M. LUNDAMEMUUNGANO0715987554
6SHADHILI NAMBAILAMEMNYEU0683660061
7HAMISI LUTAVIMENAKAHAKO0658564639
8THOMAS M. ALEXANDERMEMKOMA II0754382651
9MARIA S. NDAHELEWEKEMDIMBA0717180668
10BULENGE MWASEBAMEMNYAMBE0712233826
11GOODLUCK H. KISHIMBOMEMTOPWA0712408286
12ORGENES J. MSHANAMEMIKUMBI0675903103
13SHARIFU S. NALINGAMEMAPUTI0715860900
14PASCHAEL N. MAGUBIKAMENANDWAHI0714986198
15PETRO D. LILUNGULUMECHILANGALA0788423111
16SAADA C. ADAMKEMCHEMO0673587801
17SAID A. JUMAMENAMBALI0715133940
18SALUMU M.MOHAMEDIMECHITEKETE0788231201
19SHABANI M. NANGUKAMECHIHANGU0716154450
20SOPHIA KINYONTOKEMPWAPWA0712537732
21SWALEHE M. HASHIMUMEMAKUKWE0784225954
22YONAS S. NG’ONYEMEMALATU0757622085
JEDWALI NAMBA 3. ORODHA YA WAKUU WA SHULE
NA.NAMBA YA USAJILI
JINA LA SHULE
KATA SHULE ILIPO
JINA LA MKUU WA SHULE
NAMBA YA SIMU
1S.5013CHIHANGUCHIHANGUHADIJA N. YAHAYA0625302433
2S.3732CHITEKETECHITEKETEJOSEPH K. LUGANO0717721429
3S.3763LENGOLENGOFREDY M. JOHN0784766915
4S.3781MAKUKWEMAKUKWECHRISTOPHER A. KAYOMBO0621934337
5S.3615MALATUMALATUWAKATI N. MTOTA0679204722
6S.1654MAPUTIMAPUTIHAMIDU A. LIKULU0657217479
7S.4005MIKUMBIMIKUMBIERICK S. AWIT0716219532
8S.4267MKOMAMKOMADANIEL E. LUKUWI0784977439
9S.3696MMULUNGACHIWONGASHAFII I. MNYALU0685834444
10S.0746MNYAMBEMNYAMBEISSA M. MKUTI0652838425
11S.4102MPELEPELEMDIMBAJUSTINE K. MAGESA0629041626
12S.3767MPOTOLAKITANGARILEONARD D. KULWA0786271718
13S.3607MTOPWAMTOPWAGABRIEL C. HAULE0656401193
14S.1807USHIRIKAMKWEDUERICK L. NANDONDE0713342619
15S.2920VIHOKOLINANDWAHILUFINGO T. MWAIJANDE0689851755
16S.0999KITANGARIKITANGARIMBARAKA 0714621285
Halmashauri ya Wilaya ya Newala ina jumla ya shule za sekondari 16 ambazo wanafunzi wake walifanya mitihani ya kumaliza Elimu ya sekondari kidato cha Pili na Nne kwa miaka ya 2013, 2014, 2015, 2016, 2017, 2018 na 2019. Halmashauri pia inayo shule ya sekondari ya kidato cha 5 na 6 ambayo wanafunzi wake walifanya mitihani ya Taifa kidato cha Sita kwa miaka ya 2018 na 2019.
Matokeo ya mitihani hiyo yanaoneshwa hapa chini;-
MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MNYAMBE SEKONDARI
MWAKAWALIOANDIKISHWA
WALIOFANYA
WALIOFAULU% YA UFAULU
WALIOFELI% YA WALIOELINAFASI KIMKOANAFASI KITAIFA
2018202020100--256
2019303030100--12377
HALMASHAURI YA WILAYA YA NEWALA
MUHTASARI WA MATOKEO YA MITIHANI YA TAIFA (CSEE) KUANZIA MWAKA 2013 HADI 2019
NAMWAKA Uchambuzi wa Madaraja ya Ufaulu ya wanafunziUfaulu Drj.
1-4%
WaliofanyaDaraja la IDaraja la IIDaraja la IIIJumla Daraja la I - IIIDaraja la IVWaliofeli
WVWSJMLWVWSJMLWVWSJMLWVWSJMLWVWSJML%WVWSJML%WVWSJML%
12013255226481101707204242843279982181381281402685644
22014308218526000102121278902280102191441112554878911693268
320152652755401015055075756763121441643085768981663169
42016309310619202121135212646613791317014631651731512243664
520172161643802021631936145054177119130108238633239711981
620183163716872022122353177076199514207296503733356891387
720194084618695274310538835123136471832125936762672135366892
HALMASHAURI YA WILAYA YA NEWALA
MUHTASARI WA MATOKEO YA MITIHANI YA TAIFA YA UPIMAJI (FTNA) KUANZIA MWAKA 2013 HADI 2019
NAMWAKA Uchambuzi wa Madaraja ya Ufaulu ya wanafunziUFAULU DAR 1- 4 %
WaliofanyaDaraja la IDaraja la IIDaraja la IIIJumla Daraja la I - IIIDaraja la IVWaliofeli
WVWSJMLWVWSJMLWVWSJMLWVWSJMLWVWSJML%WVWSJML%WVWSJML%
1201385179716480000000000000305412717445463859315644
220143563637190000000000000311327638894536811189
32015248230478808281442463480824813027147136283592144651486
4201640552292761715520576111878671451634740675381611161771981
520175436781221184223774473541271286519316312474786641031392422080
620184766331109306364824721071012081851313162825844470263365591892
7201952765311802342775281031401653052381974353725943469359163854595
10.0 HALI YA MIUNDOMBINU MASHULENI
10.1 Hali ya Miundombinu
Na.Aina ya MiundombinuMahitajiIliyopoUpungufu% ya Upungufu
1Ofisi za walimu45331227
2Vyumba vya madarasa1461281812
3Nyumba za Walimu159619862
4 Vyoo vya walimu49301939
5Matundu ya Vyoo (WAV)133874635
6Maabara45172862
7Matundu ya Vyoo (WAS)144916042
8Maktaba1500100
9Stoo157853
10.1.2 Hali ya Samani:
Na.AinaMahitajiYaliyopoUpungufu% ya Upungufu
1Meza za wanafunzi5,2725,087185
4
2Viti vya wanafunzi52895,0272625
3Viti vya Walimu18017284.4
4Meza za Walimu18017284.4
5Kabati77304761
11.0 CHANGAMOTO KWA ELIMU YA SEKONDARI
•Upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi na sanaa na watumishi wengine.
•Upungufu wa miundombinu muhimu.
•Wanafunzi wanaoshindwa mtihani wa kidato cha pili kukataa kukariri darasa na kuamua kuacha shule.
•Tatizo la utoro kwa wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne
10.1HATUA ZINAZOCHUKULIWA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO
•Halmashauri kuendelea kukamilisha maabara na miundombinu mingine kadri fedha zinapopatikana.
•Kufuatilia ufundishaji na ujifunzaji shuleni ili kuinua ufaulu kwa wanafunzi
•Kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa elimu ili kuwahimiza watoto wao kuhudhuria masomo
MAWASILIANO YA IDARA
Kwa mawasiliano , maswali na maelekezo idara inatumia njia zifuatazo;-
1.Sanduku la barua - Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji (W)
Idara ya Elimu Sekondari
S.L.P 16
NEWALA – MTWARA
3.Namba za simu: 0689 533445 (DSEO)
4.Fax; 0232410211
NB. Unaweza pia kuwasiliana na Maafisaa wa Idara kupitia namba zao katika simu za
mkononi kama zilivyotolewa hapo juu.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa