Wilaya ina eneo la ardhi la jumla ya kilomita za mraba 2,126 ambapo eneo lote limefunikwa na ardhi kavu tu. Wilaya ya Newala ni wilaya ya nne kwa ukubwa wa eneo baada ya Wilaya ya Nanyumbu, Masasi na Mtwara; inachukua asilimia 12.7 ya eneo lote la Mkoa wa Mtwara. Halmashauri ya Wilaya ya Newala iko kusini mashariki mwa Tanzania kati ya longitudo 39 o - 40o Mashariki na latitudo 10o -11o kusini. Imepakana upande wa Magharibi na wilaya ya Masasi, kuelekea Mashariki na wilaya ya Tandahimba, kuelekea kaskazini na Mkoa wa Lindi na kusini na Mto wa Ruvuma ambao pia ni mpaka wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Msumbiji.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa