• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Newala District Council
Newala District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Newala

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ujenzi
      • Planning, Statistics and Coordination
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • KIlimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • ICT & Public Relations
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Usambazaji
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
      • TASAF
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba

BAJETI MPYA NEWALA DC

Posted on: February 12th, 2026

AFISA MIPANGO AWASILISHA RASIMU YA BAJETI YA SHILINGI BILIONI 25.7 NEWALA DC.


imeandikwa na Afisa Habari Shabani Mkumba 


Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Bw. Sylvester Ngonyani, amewasilisha Rasimu ya Mpango na Bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027 yenye jumla ya Shilingi Bilioni 25.7 katika kikao maalum cha Baraza la Madiwani kilichofanyika Februari 11, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri.


Akiwasilisha rasimu hiyo, Bw. Ngonyani alisema kati ya kiasi hicho, Shilingi Bilioni 13.7 zinatokana na Ruzuku ya Mishahara, Shilingi Bilioni 3.8 ni Mapato ya Ndani ya Halmashauri, Shilingi Bilioni 1.3 ni Mchango wa Jamii, na Shilingi Bilioni 6.8 ni Ruzuku kwa Miradi ya Maendeleo kutoka Serikali Kuu na Wadau wa Maendeleo.


Alieleza kuwa bajeti hiyo imelenga kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za jamii, kuimarisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo, na kukuza uchumi wa wananchi wa Wilaya ya Newala. Aidha, kwa mwaka wa fedha 2026/2027, mapato ya ndani yanatarajiwa kuongezeka kwa Shilingi Milioni 161.5, sawa na asilimia 4.2, kutoka Shilingi Bilioni 3.7 za mwaka 2025/2026 hadi Shilingi Bilioni 3.8.


Bw. Ngonyani alisema ongezeko hilo linatokana na juhudi za kuimarisha vyanzo vya mapato kama ushuru wa korosho ghafi, ada za biashara, kodi ya majengo, pamoja na mapato yanayotokana na hospitali na vituo vya afya.

Akihitimisha, Afisa Mipango huyo alisisitiza umuhimu wa kuongeza ufanisi katika ukusanyaji wa mapato, uwajibikaji wa watendaji, na matumizi sahihi ya fedha za umma ili kufanikisha utekelezaji wa bajeti na kuinua ustawi wa wananchi wa Wilaya ya Newala.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -HALMASHAURI YA WILAYA YA NEWALA December 29, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILII WA MAHOJIANO January 06, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2021 MNYAMBE SEKONDARI July 10, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 22, 2022
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • DC KUNDYA AKABIDHI MSAADA KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUM

    February 13, 2026
  • LANDSBERG UJERUMANI YAENDELEA KUCHANGIA MAENDELEO NEWALA DC

    February 13, 2026
  • BAJETI MPYA NEWALA DC

    February 12, 2026
  • BAJETI YA NEWALA DC BILIONI 25.7 KWA MWAKA 2026/2027

    February 12, 2026
  • Ona Zote

Video

Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Historia ya Halmashauri
  • Idara ya Rasilimali Watu

Kurasa mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Poralg
  • Secretariet ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Kitangari,Newala

    Anuani ya Posta: P.O. Box 16

    Simu: +255232410251

    Mobile:

    Barua pepe: ded@newaladc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma zetu

Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa