ZAIDI YA WATU 8,000 KUNUFAIKA NA KITUO KIPYA CHA AFYA NANDWAHI
Halmashauri ya Wilaya ya Newala imekamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Nandwahi kwa kutumia shilingi milioni 250 zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kwa mujibu wa idadi ya watu katika Kata ya Nandwahi, mradi huo utanufaisha takribani wananchi zaidi ya 8,133 wanaotarajiwa kupata huduma bora za afya karibu na makazi yao.
Wananchi wa Kata ya Nandwahi wamefurahishwa na kukamilika kwa ujenzi huo, wakimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma za afya vijijini na kusogeza huduma karibu na wananchi. Wamesema kituo hicho kitapunguza changamoto za umbali na gharama walizokuwa wakizipata kufuata matibabu katika maeneo ya mbali.
#KaziNaUtuTunasongaMbele
Kitangari,Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa