NEWALA, MTWARA
Halmashauri ya wilaya ya Newala Jana Oktoba 30,2024 imeadhimisha siku ya Lishe kitaifa katika Kijiji cha Makukwe ikiwa na kauli mbiu isemayo "Mchongo ni Afya yako, zingatia unachokula"
Maadhimisho hayo yamefanyika yakiwa na lengo la kutoa elimu ya Lishe kwa jamii kwa kuzingatia mapendekezo ya mwongozo wa kitaifa wa chakula na ulaji unaofaa kwa Afya Bora
Aidha wataalam wa Afya na Lishe wametoa elimu ya nadharia ikiwemo maana ya Lishe Bora,umuhimu wa chanjo na jiko darasa kwa vitendo ambapo Jamii imejifunza mapishi ya uji ulioboreshwa wenye makundi 6 ya vyakula muhimu kwa ajili ya kukua vyema, kujenga mwili lakini pia kuimarisha Kinga ya mwili.
Akitoa elimu, Afisa lisha wilaya Bi Christina Lukinisha amesema ili lishe iwe Bora ni muhimu iwe na mchanganyiko wa vyakula mbalimbali kama vile protini kutoka kwenye nyama na Jamii ya kunde ,vyakula vya wanga, mbogamboga, mafuta, madini , matunda na maji kwa wingi.
Amesema licha ya watu wengi kujua umuhimu wa Lishe Bora lakini imekuwa tofauti kwa baadhi ya familia nyingi kwani kumekuwa na tabia ya kula chakula cha aina moja ambapo inasababisha watu kuwa na hali duni kiafya ambayo ndio chanzo cha magonjwa mbalimbali hatari.
" Nitoe rai kwa wananchi kujenga utamaduni wa kula Lishe Bora yenye mchanganyiko wa vyakula mbalimbali kwani inasaidia kupunguza vifo vya watoto vinavyotokana na Lishe duni" Amesema Lukinisha
Aidha huduma za Afya zilizotolewa kwa katika maadhimisho ni Pamoja naTathmini ya Hali ya lishe na upimaji wa hali ya lishe na magonjwa yasiyoambukizwa,Elimu ya ulaji unaofaa kutoka makundi sita ya chakula,Jiko darasa,huduma za afya ikiwemo umuhimu wa chanjo na kumaliza chanjo,huduma za ustawi wa jamii,umuhimu wa wajawazito kuwahi kliniki, upimaji wa saratani ya shingo ya uzazi na uchangiaji wa damu.
Wataalam wa Afya walioshiriki katika utoaji wa huduma za afya na Elimu ni Christine Rukinisha- Afisa Lishe wa Wilaya,Jane Mgaza - Afisa Lishe, Stelina Ndokole- Afisa Chanjo,Jamila Nalinga - katibu wa afya na Saidi Mwengele Afisa Afya
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa