Kuelekea zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura awamu ya pili linalotarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 2 hadi 4 Mei 2020, Halmashauri ya Wilaya ya Newala leo imetoa mafunzo elekezi kwa wasimamizi wasaidizi 22 ngazi ya kata, waandishi wasaidizi na waendeshaji wa mashine za kujiandikisha (BVR Kits operators) 46.
Akifungua mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Mussa Chimae amewataka wasimamizi wa zoezi hilo kuchukua tahadhari ya maambukizi ya virusi vya Corona katika kipindi chote cha uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kuhakikisha wananchi wote kunawa maji tiririka na sabuni kabla ya kupata huduma, kuzingatia umbali wa kukaa kati ya mtoa huduma na anayehudumiwa, kusafisha mashine kwa spirit na kuvaa barakoa katika muda wote wa zoezi hilo.
Katika zoezi hilo, wananchi watakuwa na nafasi ya kuhakiki majina yao na kuhuisha taarifa zao pale inapohitajika katika vituo 22 ambapo kila kata itakuwa na kituo kimoja.
Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata wakila kiapo mbele ya Mhe.Hakimu wa mahakama ya mwanzo Kitangari Mussa Omari Nambunga.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa siku moja leo tarehe 30 Aprili 2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha walimu Kitangari yakiambatana na kiapo kwa wasimamizi wote wa zoezi hilo na mafunzo yameendeshwa na maafisa TEHAMA wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala wakishirikiana na wataalamu kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa