NEWALA
Mkuu wa wilaya ya Newala Mhe.Rajabu Kundya amekabidhi vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu katika Halmashauri ya wilaya ikiwemo viti vya magurudumu 7 magongo,baiskeli za mataili matatu 10 na fimbo nyeupe vyenye thamani ya shilingi Milioni 11.7 ikiwa ni Msaada kutoka Hospitali ya Rufaa Ndanda chini ya Ufadhili wa marafiki wa Ujerumani.
Vifaa hivyo ambavyo vitatumika kutatua changamoto zinawakabili katika maisha ikiwemo kutembea,vimekabidhiwa Jana Desemba 10,2024 katika maadhimisho ya kimataifa ya watu wenye ulemavu yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Kitangari Mazoezi yakiwa na kauli mbiu isemayo" kukuza uongozi wa watu wenye ulemavu kwa ajili ya mstakabali wa jumuishi na Endelevu"
Akihutubia wananchi na wageni mbalimbali walioshiriki maadhimisho hayo Mkuu wa wilaya Mhe Kundya ameishukuru Taasisi ya Ndanda Hospital Pamoja na marafiki wa ujerumani kwa misaada yao mingi na mikubwa ambayo wanaitoa.
" Nichukue nafasi hii kuwaomba na kuwasihi wasituchoke,waendelee,kuwasaidia watu wetu maana ukiweka tabasamu kwa mtu mwenye mahitaji maalumu utakuwa umetenda jambo jema hata Mwenyezi Mungu hasiti kuweka tabasamu kwenye uso wako" Amesema Kundya
Aidha ametoa wito na kuwaomba watu wa Newala kuwa na moyo wa kupenda kuwasaidia watu wenye ulemavu ili waondokane na changamoto ndogondogo zinazowakabili katika maisha yao.
Kwa upande wao baadhi ya wanaufaika akiwemo Salmini Saidi,mwanafunzi wa kidato tano mwenye ulemavu wa viungo na Zahana Abdala ambaye ni shangazi wa salafina bashiri mwenye ulemavu wa viungo wamefurahia na kushukuru msaada uliotolewa na Halmashauri kwa ushirikiano na Hospitali ya Rufaa Ndanda na watu wa ujerumani.
Wamesema vifaa hivyo saidizi vitawasaidia kutembea kwa urahisi na kufanya shughuli mbalimbali za kuendesha maisha yao.
Halmashauri ya Wilaya ya Newala ina watu wenye walemavu wapatao 821 kati ya hao watoto ni 235.
@ortamisemi
@dc_newala
@msemajimkuuwaserikali
@mtwarars_habari
@maendeleoyajamii
@kundya_mwangi
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa