• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Newala District Council
Newala District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Newala

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ujenzi
      • Planning, Statistics and Coordination
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • KIlimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • ICT & Public Relations
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Usambazaji
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
      • TASAF
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba

Watumishi wa umma wa Mkoa wa Mtwara watakiwa kuwajibika vyema katika maeneo yao ya kazi.

Posted on: May 1st, 2021

Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani katika Mkoa wa Mtwara leo tarehe 01/05/2021 yamefanyika katika kiwanja cha shule ya msingi Amani iliyopo katika Wilaya ya Tandahimba.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mhe. Sebastian Waryuba, Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa.

Katika maadhimisho hayo, Mhe. Waryuba amewataka watumishi kuwajibika vyema katika kazi zao ili maslahi bora wanayoyadai yaendane na utendaji wao wa kazi, kama kauli mbiu ya siku ya wafanyakazi duniani kwa nchi ya Tanzania mwaka huu 2021 inavyosema "Maslahi bora, mishahara juu. Kazi iendelee."

Sherehe za madhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mkoa wa Mtwara zimeenda sambamba na kuwatambua wafanyakazi bora wa Ofisi za Mikoa, Halmashauri, Taasisi za Serikali na mashirika ya umma ambapo walipatiwa vyeti vya kuwatambua na zawadi ikiwa ni hamasa ya wafanyakazi hao na wengine kufanya vizuri zaidi katika majukumu yao maeneo yao ya kazi.

Watumishi bora wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala kwa mwaka 2021, wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa vyeti vyao vya pongezi pamoja na zawadi kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani, Mkoa wa Mtwara.

Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala jumla ya watumishi bora 16 kutoka idara za Utumishi na Utawala, Fedha, Kilimo, Afya, Maendeleo ya jamii, Ujenzi, Mifugo, Elimu Msingi na Elimu Sekondari walitambuliwa na kupatiwa vyeti na zawadi.

Sherehe ya maadhimisho hayo ilihudhuriwa na wakuu wa wilaya za mkoa wa Mtwara; makatibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara; Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Wilaya na Miji, Wenyeviti wa Halmashauri zote za mkoa wa Mtwara; viongozi wa vyama vya wafanyakazi; wakuu wa taasisi na mashirika,  watumishi, waandishi wa habari na wananchi.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -HALMASHAURI YA WILAYA YA NEWALA December 29, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILII WA MAHOJIANO January 06, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2021 MNYAMBE SEKONDARI July 10, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 22, 2022
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • MWEZI WA AFYA NA LISHE KWA WATOTO

    July 04, 2025
  • UJUMBE WA SHUKRANI KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    July 04, 2025
  • NEWALA DC YAPOKEA MITUNGI YA GESI

    June 24, 2025
  • MKUTANO MAALUM WA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI

    June 21, 2025
  • Ona Zote

Video

Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Historia ya Halmashauri
  • Idara ya Rasilimali Watu

Kurasa mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Poralg
  • Secretariet ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Kitangari,Newala

    Anuani ya Posta: P.O. Box 16

    Simu: +255232410251

    Mobile:

    Barua pepe: ded@newaladc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma zetu

Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa