• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Newala District Council
Newala District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Newala

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ujenzi
      • Planning, Statistics and Coordination
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • KIlimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • ICT & Public Relations
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Usambazaji
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
      • TASAF
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba

NEWALA DC YAPOKEA MITUNGI YA GESI

Posted on: June 24th, 2025

RAIS SAMIA AWASUKUMA NEWALA DC KWENYE NISHATI SAFI :MAJIKO YA GESI kWA BEI YA RUZUKU


Imeandikwa na Afisa Habari Shabani Mkumba.


 Serikali kupitia Mradi wa Taifa wa Nishati Safi kwa Kupikia unaoratibiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imeipatia Halmashauri ya Wilaya ya Newala jumla ya mitungi 1,780 ya gesi ya kupikia, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maono ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanatumia nishati salama na rafiki kwa afya na mazingira.


Akizungumza leo Juni 23, 2025 katika ofisi ya Halmashauri  wakati wa zoezi la ugawaji wa mitungi hiyo kwa wananchi, Afisa Usafi na Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Ndugu.Tumaini Sadick, alisema kuwa utekelezaji wa mpango huo ni hatua muhimu katika kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ambayo yamesababisha athari za kiafya na kimazingira kwa muda mrefu.


 “Kupitia mradi huu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, Halmashauri ya Newala tumepokea mitungi 1,780 ya gesi kwa ajili ya wananchi. Mitungi hii inatolewa kwa bei ya ruzuku ambapo mwananchi anachangia shilingi 19,500 na serikali inachangia kiasi hicho hicho, hivyo kufanya gharama kuwa shilingi 39,000 tu kwa kila jiko,” alisema Ndugu Sadick.


Alieleza kuwa mitungi hiyokutoka Kampuni ya Taifa Gesi  imeanza kugawiwa kwa wananchi waliopo kwenye mpango huo katika vijiji mbalimbali, kwa kushirikiana na kitengo cha maliasiri na hifadhi za mazingira huku elimu ya matumizi salama ya gesi ikiendelea kutolewa.


Ndugu. Sadick alisisitiza kuwa matumizi ya gesi yatasaidia kulinda au kupunguza  magonjwa dhidi ya moshi unaotokana na kuni, sambamba na kupunguza uharibifu wa mazingira unaotokana na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa.


Aidha, alitoa shukrani kwa Serikali kwa kuwezesha upatikanaji wa majiko haya kwa ruzuku, akisema kuwa hatua hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wananchi wa vijijini wanaotegemea kuni kama chanzo kikuu cha nishati ya kupikia.

@mtwarars_habari

@samia_suluhu_hassan

@msemajimkuuwaserikali

@ortamisemi

@dc_newala

https://www.instagram.com/p/DLQfrctooQr/?igsh=aHRscGl4enN1OHMz

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -HALMASHAURI YA WILAYA YA NEWALA December 29, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILII WA MAHOJIANO January 06, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2021 MNYAMBE SEKONDARI July 10, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 22, 2022
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • NEWALA DC YAPOKEA MITUNGI YA GESI

    June 24, 2025
  • MKUTANO MAALUM WA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI

    June 21, 2025
  • MKUTANO MAALUM WA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI

    June 21, 2025
  • MKUTANO MAALUM WA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI

    June 21, 2025
  • Ona Zote

Video

Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Historia ya Halmashauri
  • Idara ya Rasilimali Watu

Kurasa mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Poralg
  • Secretariet ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Kitangari,Newala

    Anuani ya Posta: P.O. Box 16

    Simu: +255232410251

    Mobile:

    Barua pepe: ded@newaladc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma zetu

Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa