Jumla ya watoto 15,275 wenye umri wa miezi 6 hadi 59 wamepatiwa matone ya Vitamin A katika Halmashauri ya Wilaya ya Newala, sawa na asilimia 97 ya lengo lililowekwa.
Taarifa hiyo imetolewa na Afisa Lishe wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Bi. Jane Mgaza, ambaye amesema zoezi hilo limefanyika kwa mafanikio makubwa kupitia uhamasishaji na utoaji elimu kwa Jamii katika Mwezi wa Afya na Lishe kwa watoto wadogo.
Bi. Mgaza amesema kuwa utoaji wa Vitamin A ni hatua muhimu katika kuimarisha afya ya mtoto, kuongeza kinga ya mwili,kusaidia ukuaji na uimara wa meno na mifupa pamoja na kupunguza vifo vinavyotokana na magonjwa mbalimbali.Aidha katika zoezi hilo watoto walipata dawa za minyoo na kupimwa urefu ambapo watoto 5,971 wanatarajia kufikiwa kwa kupimwa urefu ifakapo Julai 13,2025.
Hii ni sehemu ya mikakati ya Halmashauri kuhakikisha watoto wanapata lishe bora na kinga dhidi ya maradhi, ili wakue katika mazingira salama na yenye afya.
@ortamisemi
@mtwarars_habari
@msemajimkuuwaserikali
@wizara_afyatz
@newalafmtz
@dc_newala
https://www.instagram.com/p/DLpN_lNoRpt/?igsh=OXN6emgyNW1oNXBs
Kitangari,Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa