UJUMBE WA SHUKRANI KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Halmashauri ya Wilaya ya Newala inamshukuru kwa dhati Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutupatia jumla ya watumishi wapya 202 kutoka kada mbalimbali kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Kupokelewa kwa watumishi hawa ni ushahidi tosha wa dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita katika kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi, kuongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuleta chachu ya maendeleo endelevu katika Halmashauri yetu.
Watumishi hawa wataongeza nguvu kazi katika sekta muhimu kama afya, elimu, kilimo, maendeleo ya jamii, utawala na sheria, na hivyo kusaidia kwa kiwango kikubwa kuinua ustawi wa jamii ya wananchi wa Newala.
Kwa moyo wa shukrani, tunasema: "Asante sana Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutujali, kutusikia na kutujengea matumaini mapya. Tunaahidi kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na weledi mkubwa kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla."
@mtwarars_habari
@msemajimkuuwaserikali
@samia_suluhu_hassan
@newalafmtz
@dc_newala
@ortamisemi
Kitangari,Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa