• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Newala District Council
Newala District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Newala

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ujenzi
      • Planning, Statistics and Coordination
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • KIlimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • ICT & Public Relations
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Usambazaji
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
      • TASAF
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba

Kamati za ulinzi na usalama wa mtoto Newala zajengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yao.

Posted on: June 22nd, 2021

Kamati za ulinzi na usalama wa mwanamke na mtoto kutoka katika kata za Halmashauri ya Wilaya ya Newala zajengewa uwezo wa kutekeleza majukumu yao leo tarehe 22/06/2021 kwa kupitia kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha walimu Kitangari. 

Majukumu ya kamati hizo za ulinzi wa mama na mtoto ni kusimamia mpango kazi wa kijiji na kata na kuandaa taarifa zote za utekelezaji wa mpango; kutambua na kusajili watoto wote wanaoishi katika mazingira hatarishi; na kutoa taarifa kwenye mamlaka husika iwapo yatatokea maswala ya kikatili yanayofanywa kwa wanawake na watoto.

Akifungua kikao kazi hicho, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bi. Magreth Likonda amewataka washiriki wote kuzingatia maelekezo watakayopewa kwa kuwa wao ni watu muhimu sana katika usimamizi wa haki za wanawake na watoto kwa kuwa ni miongoni mwa jamii hiyo.

"Nyinyi kama wawakilishi wa jamii, mmepewa dhamana ya kusimamia ulinzi na usalama wa mwanamke na mtoto, mkahakikishe mnatekeleza majukumu yenu vyema kwa kuibua na kukemea viashiria vyote vya ukatili huo katika jamii". Alisema Bi. Likonda.

Kamati hizi zipo katika ngazi ya Taifa, Mkoa, Halmashauri,  Kata na Kijiji zenye jukumu la kutokomeza  maswala yote yanayohusu ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Aidha, baada ya kikao kazi hicho, wajumbe wa kamati hiyo watakuwa na zoezi la kuwatambua watoto wenye mahitaji maalum katika mazingira wanayotoka kwa kuwa jamii kwa ujumla ina jukumu la kuhakikisha mtoto analindwa na anaishi katika mazingira salama.

Mratibu wa Mpango wa Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWA) Newala Bw. Bakari Mnali, akitoa mafunzo kwa wajumbe wa MTAKUWA ngazi ya Kata.

"Hii iwe chachu ya Watendaji wa Kata na Vijiji ambao ndiyo wasimamizi wa MTAKUWA katika maeneo yenu, kuona namna shughuli za Ustawi wa jamii zinaingia katika utekelezaji wa shughuli zao za kila siku na taarifa zake ziwe zinaingia katika taarifa za vijiji za kila mwezi na taarifa za kata za kila baada ya miezi mitatu." Alisema Bw. Mnali, Mratibu wa Mpango wa Kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (MTAKUWA) Halmashauri ya Wilaya ya Newala. 

Kikao kazi hicho ni cha siku tatu, kuanzia tarehe 22 hadi 24/06/2021.



































Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -HALMASHAURI YA WILAYA YA NEWALA December 29, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILII WA MAHOJIANO January 06, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2021 MNYAMBE SEKONDARI July 10, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 22, 2022
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • MWEZI WA AFYA NA LISHE KWA WATOTO

    July 04, 2025
  • UJUMBE WA SHUKRANI KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    July 04, 2025
  • NEWALA DC YAPOKEA MITUNGI YA GESI

    June 24, 2025
  • MKUTANO MAALUM WA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI

    June 21, 2025
  • Ona Zote

Video

Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Historia ya Halmashauri
  • Idara ya Rasilimali Watu

Kurasa mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Poralg
  • Secretariet ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Kitangari,Newala

    Anuani ya Posta: P.O. Box 16

    Simu: +255232410251

    Mobile:

    Barua pepe: ded@newaladc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma zetu

Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa