Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Mussa Chimae amefanya ziara ya kikazi siku ya Jumatatu tarehe 15/07/2019 ya kutembelea pango la Nadululu lililopo kijiji cha Chilangala, kata ya Chilangala, Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Ziara hiyo ameifanya akiambatana na timu ya menejimenti ya Halmashauri iliyohusisha wakuu wa idara na vitengo vyote vilivyopo kwenye Halmashauri hiyo.
Bw. Chimae amefanya ziara hiyo kwa lengo la kubaini na kukagua sehemu za utalii zilizopo kwenye eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Newala na kuzitangaza sehemu hizo ili zifahamike na watu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Newala.
Pango la Nadululu ni pango la asili na la kihistoria ambalo lina mawe mengi ya thamani, chemchemi za maji zisizokauka na zenye maji yanayotumika kunywa, na yanayosadikiwa kutibu magonjwa mbalimbali, miti ya asili yenye magome yanayoweza kutumika kufulia nguo kama sabuni na kutengenezea manukato, na mawe yanayotoa chumvi.
Sehemu za utalii ni muhimu kwa maeneo mbalimbali kwa kuwa hutunza historia na kukuza uchumi wa eneo husika, jamii inayozunguka eneo hilo, Halmashauri, Wilaya na Taifa kwa ujumla.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa