TAARIFA KWA UMMA
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala anawataarifu wananchi wote kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala imepokea kiasi cha shilingi 850,000,000.00 kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia mpango wa Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.
Fedha hizi zitatumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Sekta za Elimu, Afya na Utawala, ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Newala inaendelea kusisitiza mshikamanano na ushirikiano wa wananchi wote katika kuhakikisha miradi hii inatekelezwa kwa ufanisi na kwa manufaa ya jamii.
“Kazi na utu tunasonga mbele”
Natanguliza shukrani.
NDUGU DUNCAN THEBAS
Mkurugenzi Mtendaji
Halmashauri ya Wilaya ya Newala (Newala DC)
Kitangari,Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa