• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Newala District Council
Newala District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Newala

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ujenzi
      • Planning, Statistics and Coordination
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • KIlimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • ICT & Public Relations
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Usambazaji
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
      • TASAF
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba

Newala DC yawarejesha watendaji 56 kazini

Posted on: August 7th, 2018

Halmashauri ya Wilaya ya Newala imewarejesha kazini watendaji 56 wa vijiji ikiwa ni pamoja na kuwarejesha katika malipo yao ya mishahara kama ilivyo kawaida.

Akitoa taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala katika mkutano wa baraza la madiwani uliofanyika tarehe 7/8/2018 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bwana Nsajigwa Sadick, amesema watendaji wa vijiji waliorejeshwa kazini ni wale waliotolewa kwa kukosa sifa ya Elimu ya kidato cha nne kutokana na maelekezo ya katibu mkuu Utumishi, na tayari wameshapangiwa vituo vya kazi,ambapo wanatakiwa waripoti katika vituo hivyo kabla ya tarehe 8/8/2018.

Wakati huo huo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Mhe.Chitwanga Rashid Ndembo amesema katika mwaka wa fedha wa 2017/2018, Halmshauri ya Wilaya ya Newala imetekeleza miradi kwa asilimia 40 tu kutokana na uwezo wa Halmashauri kupitia mapato ya ndani ambayo yaliathirika kutokana na ukosefu wa soko la mbaazi pamoja na ukosefu wa vyanzo vingine vya mapato ikiwa ni pamoja na serikali kupunguza tozo ya  ushuru wa korosho au ushuru wa mazao ya biashara kutoka asilimia 5 hadi asilimia 3, kwani Halmashauri ilipanga bajeti yake kwa kuzingatia asilimia 5 ya ushuru wa korosho, hivyo kutokana na kupunguzwa kwa asilimia hizo kumepelekea kuathiri malengo ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kufuatia hilo Halmashauri imejipanga vizuri kuhakikisha inakusanya mapato kwa wingi kupitia mashine za kukusanyia mapato ya halmashauri (POSS) ili kuweza kufanikisha malengo ya halmashauri ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vingine mbalimbali vya mapato.

Katika hatua nyingine Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Newala, limefanya uchaguzi wa viongozi na wajumbe wa kamati za kudumu za Halmashauri ya Wilaya ya Newala, na kumchagua Makamu Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Mhe.Rashidi Songoni wa CCM, aliyeshinda kwa kura 27 kati ya 29 dhidi ya mpinzani wake Mhe.Simon Nchingulu wa CUF, na kutangazwa na baraza kuwa ndiye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri kuanzia tarehe 7/8/2018.

Mhe.Rashidi Songoni (wa mbele kabisa) Makamu Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala alipokuwa akiomba kura kwa wajumbe wa baraza mapema kabla ya uchaguzi wa makamu Mwenyekiti uliofanyika tarehe 7/8/2018 katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya Wilaya ya Newala.

Mhe.Songoni amechukua nafasi hiyo iliyokuwa inashikiliwa na Mhe.Swalehe Fakihi (CCM) kwa zaidi ya miaka miwili.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -HALMASHAURI YA WILAYA YA NEWALA December 29, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILII WA MAHOJIANO January 06, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2021 MNYAMBE SEKONDARI July 10, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 22, 2022
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • NEWALA DC YAPOKEA MITUNGI YA GESI

    June 24, 2025
  • MKUTANO MAALUM WA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI

    June 21, 2025
  • MKUTANO MAALUM WA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI

    June 21, 2025
  • MKUTANO MAALUM WA KUVUNJA BARAZA LA MADIWANI

    June 21, 2025
  • Ona Zote

Video

Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Historia ya Halmashauri
  • Idara ya Rasilimali Watu

Kurasa mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Poralg
  • Secretariet ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Kitangari,Newala

    Anuani ya Posta: P.O. Box 16

    Simu: +255232410251

    Mobile:

    Barua pepe: ded@newaladc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma zetu

Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa