NEWALA DC YANUFAIKA NA JENGO LA UTAWALA,WATUMISHI WAPONGEZA UONGOZI WA RAIS SAMIA.
Watumishi wa umma Halmashauri ya wilayani Newala wamepongeza jitihada za serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwajengea jengo jipya la utawala lenye thamani ya shilingi BIlioni 2.75, hatua ambayo imerahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi.
Kabla ya uwepo wa jengo hilo, ofisi za idara mbalimbali zilikuwa zilikuwa katika sehemu tofauti, hali iliyosababisha usumbufu kwa wananchi waliokuwa wakihitaji huduma tofauti.
Wakizungumza kuhusu maendeleo ya kipindi cha Miaka 4 ya uongozi wa Rais Samia, watumishi hao wa serikali wamesema kuwa ujenzi wa jengo hilo umewapa mazingira bora ya kazi na kuimarisha utoaji wa huduma.
"Kwa kweli, tunaishukuru sana serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutujengea jengo hili la utawala. Zamani tulikuwa tunahangaika kutafuta huduma kwenye ofisi zilizotawanyika, lakini sasa ofisi zote zipo katika jengo moja. Hii imerahisisha sana utendaji kazi wetu na utoaji wa huduma kwa wananchi," walisema watumishi Deoniz na Hadija.
Kwa upande wa Wananchi waliohojiwa nao wamefurahishwa na uwepo wa jengo hilo, wakisema kuwa limepunguza muda waliokuwa wakitumia kuhangaika kufuata huduma mbalimbali.
Wamesema kuwa hatua hii inaonyesha namna serikali ya Rais Samia inavyothamini utawala bora na ustawi wa wananchi kwa kuweka mifumo bora ya utoaji wa huduma.
@ortamisemi
@mtwarars_habari
@msemajimkuuwaserikali
@maelezonews
@newalafmtz
@dc_newala
@kundya_mwangi
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa