Mkutano wa baraza la wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Newala leo tarehe 20/01/2021 umepitisha rasimu ya bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Newala kwa mwaka wa fedha wa 2021/2022 yenye jumla ya Tsh. 21,196,607,600.00
Wajumbe wa baraza la wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Newala wakiwa kwenye mkutano wa baraza hilo uliofanyika leo tarehe 20/01/2021 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha walimu Kitangari.
Akiwasilisha rasimu hiyo, Kaimu Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Benaya Sanane ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2021/2022, Halmashauri ya Wilaya ya Newala inatarajiwa kukusanya na kutumia kiasi cha Tsh. 21,095,607,600.00 kutoka katika vyanzo mbalimbali vya mapato ikiwemo ruzuku kutoka Serikali kuu, wahisani wa maendeleo na mapato ya ndani ya Halmashauri.
"kiasi hicho cha fedha kitatumika katika kulipa mishahara ya watumishi, matumizi ya kawaida, na utekelezaji wa miradi ya maendeleo" alieleza Bw. Sanane.
Wajumbe wa baraza hilo la wafanyakazi walipata nafasi ya kujadili rasimu hiyo ya bajeti na hatimaye kuridhia kuipitisha.
Mijadala hiyo ilisisitiza kuzingatia maslahi ya watumishi kwa kuyalipa kwa wakati ili kuepuka kulimbikiza madeni ambayo yanasababisha Halmashauri kushindwa kuyalipa kwa pamoja.
Mkutano huo baraza la wafanyakazi la Halmashauri ya Wilaya ya Newala umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha walimu Kitangari na umehudhuriwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Duncan Thebas, wakuu wa idara na vitengo, watumishi mmoja mmoja wawakilishi wa kila idara na vitengo vya Halmashauri, wajumbe wa vyama vya wafanyakazi wa Mkoa wa Mtwara na wawakilishi wa vyama vya wafanyakazi vilivyopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa