MILION 17.8 ZA MFUKO WA ELIMU NEWALA DC ZATUMIKA MOTISHA
Halmashauri ya wilaya ya Newala Mkoa wa Mtwara imetumia shilingi milioni 17.8 kwa ajili ya utoaji wa tuzo kwa shule na walimu waliofanya vizuri katika ufundishaji wa masomo ikiwa ni motisha baada ya wanafunzi kufaulu vizuri mitihani ya taifa kwa mwaka 2021.
Utoaji wa tuzo hizo umefanyika leo katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari Mnyambe ambapo shule bora 12 na walimu 88 wamepata zawadi ya vyeti na fedha.
Akizungumza katika sherehe hiyo mgeni rasmi Merry Twamgabo, ambaye alimwakilisha Kaimu mkuu wa wilaya ya Newala amempongeza Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Newala kwa kuwapatia motisha walimu waliofanya vizuri katika ufundishaji na kwamba kitendo hicho kitaleta hamasa zaidi ya walimu kujituma katika ufundishaji .
Aidha ameipongeza kamati ya huduma za jamii kutenga fedha kupitia mfuko wa elimu kwa ajili ya kutoa motisha ambapo amewataka walimu ambao wamekosa zawadi kujituma katika ufundishaji ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi katika mitihani ya taifa mwaka 2022.
Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Newala, Famili Mshaghira amesema Halmashauri itaendelea kuunga mkono juhudi za walimu katika ufundishaji ambapo utaratibu wa kutoa motisha utaendelea kuwepo ili kuwapa hamasa ya kujituma. Amewataka walimu kushirikiana na kufanya kazi kwa weledi ili kuleta Matokeo chanya katika ufaulu wa wanafunzi.
Aidha kwa upande wake afisa elimu sekondari,Friday Sondasy, Halmashauri ya wilaya ya Newala amesema tuzo zilizotolewa zimezingatia katika upimaji wa mitihani ya darasani la 4,Matokeo ya elimu ya msingi ,upimaji wa mitihani ya kidato cha pili na matokeo ya kidato cha nne kwa mwaka 2021.
Ameongeza kuwa zawadi ya vyeti na fedha zimetolewa kwa viongozi Bora ,shule Bora zilizo faulisha kwa 100% , walimu waliofaulisha kwa 100% na walimu waliofaulisha daraja A
Afisa Elimu Sondasy ametaja mikakati ya kuongeza ufaulu kuwa ni pamoja na kutoa motisha na kuzipitia shule zinazofanya vibaya ili kuzungumza na walimu kujua changamoto walikuwanazo na kuzitafutia ufumbuzi.
Sherehe za utoaji tuzo hii Leo zilihudhuliwa na wakuu wa shule,walimu wa taaluma ,walimu waliofanya vizuri,maafisa elimu kata ,maafisa Tarafa,wakuu wa idara,katibu wa chama Cha walimu na kamati ya ulinzi na usalama
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa