Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Newala Vijijini Bw. Duncan Thebas leo Jumatano tarehe 21/10/2020 amewaapisha mawakala wa vyama vya siasa vitakavyoshiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Rais na Madiwani unaotarajiwa kufanyika tarehe 28/10/2020.
Mawakala wa vyama vya siasa wakila kiapo cha kutunza siri mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Rais na madiwani wa mwaka 2020 Jimbo la Newala Vijijini Bw. Duncan Thebas.
Akiendesha zoezi hilo, Bw. Thebas amewataka mawakala hao kutunza siri wakati wa zoezi zima la uchaguzi na kufuata taratibu zote walizoelekezwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa kuwa wana jukumu kubwa la kuhakikisha zoezi zima la uchaguzi linafanyika kwa haki na amani.
"Kwa mujibu wa sheria kila chama kina haki ya kuweka mawakala katika kituo cha kupigia kura.
Wanaoapa leo ndio watakaokuwa kwenye vituo vya kupigia kura. Kazi yao ni kuangalia, kutambua kama taratibu zote za zoezi zima la upigaji kura zinafuatwa mpaka mwisho." Alisema Bw. Duncan.
Jimbo la Newala Vijijini ni moja ya majimbo ya uchaguzi Tanzania lenye jumla ya wapiga kura 74,041 wanaotarajiwa kushiriki zoezi la kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu.
Jimbo hili lina jumla ya vituo vya kupigia kura 216, wagombea wa ubunge wanne (4) na wagombea udiwani hamsini na nne (54) wanaotoka katika vyama vya ACT wazalendo, CCM, CHADEMA na CUF watakaoshiriki katika kuwania kupata uongozi kwenye Uchaguzi Mkuu wa Rais na madiwani wa mwaka huu 2020.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa