Halmashauri ya Wilaya ya Newala yapongezwa kwa kufanya vizuri ujenzi wa miundombinu ya kituo cha afya cha Kitangali.
Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 12/12/2019 na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw. Alphayo Kidata alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho cha afya na kukagua hali ya ujenzi wa miundombinu yake.
Mwanakamati wa kamati ya ujenzi wa kituo cha afya cha Kitangali akisoma taarifa ya mradi kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw. Alphayo Kidata alipotembelea kituoni hapo.
Ziara hiyo ilianza kwa Bw. Kidata kupokea taarifa ya mradi wa upanuzi wa kituo hicho cha afya kutoka kwa Bw.Siwatu ambaye ni mwanakamati wa ujenzi wa mradi huo ambapo aliambiwa kuwa makisio ya mradi huo ni Tsh. 432,664,011.00 ambapo Tsh. 400,000,000.00 zimetolewa na Serikali kuu, Tsh. 30,064,011.00 zinatoka Halmashauri na Tsh. 2,600,000.00 ni mchango wa wananchi.
"Ni mara ya kwanza nimetembelea vituo vya afya nikasomewa taarifa na mmoja wa wanakamati wa mradi....na hii inaonyesha nyinyi hapa ni timu moja kuliko tulipotoka, hongereni sana." Alisema Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw. Kidata.
Upanuzi wa kituo cha afya cha Kitangali umehusisha ujenzi wa majengo saba, ambayo ni jengo la upasuaji, wodi ya mama na mtoto, nyumba moja ya mtumishi, chumba cha kufulia nguo, jengo la maabara, chumba cha kuhifadhia maiti na kichomea taka.
Bw. Alphayo Kidata na wajumbe wa Sekretariet ya Mkoa wa Mtwara wakikagua wodi ya wakina mama katika kituo cha afya cha Kitangali
Kukamilika kwa mradi huo kunanufaisha wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala kwa kuwaletea karibu huduma mbalimbali ikiwemo upasuaji mkubwa na kuwaepusha wagonjwa kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 40 kwenda hospitali za Mji Newala, Ndanda na Nyangao kupata huduma hizo.
Ziara hiyo ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara Bw. Kidata kwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala ni ya kwanza tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo na ilijumuisha wataalamu wa sekta za afya na miundombinu kutoka Sekretariet ya Mkoa wa Mtwara.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa