NEWALA, MTWARA
Mfumo ulioboreshwa wa usimamizi na uendeshaji wa shughuli za Afya (GOTHOMIS) umetajwa kuwa ufumbuzi wa utendaji kazi nzuri na utoaji wa ripoti sahihi katika vituo vya kutolea huduma za Afya.
Hayo yamesemwa jana na Afisa TEHAMA Halmashauri ya wilaya ya Newala Ndugu Albano George wakati akiendesha mafunzo kwa watumishi wa Afya katika kituo cha Afya Kitangari.
" Sisi katika Halmashauri ya wilaya ya Newala, tumeweza kufunga mfumo wa Gothomis katika zahanati 13, Hospital ya wilaya na Vituo vya Afya viwili"
" Kiutendaji kazi umeweza kurahisisha utoaji wa ripoti sahihi za wagonjwa wanaotibiwa,utunzajiwa kumbukumbu na huduma nyingine zinazofanyika katika vituo vya kutolea huduma za Afya" Amesema Albano
Aidha kwa upande wa muhudumu wa zahati ya mkongi Bi Grace Lusalanya amesema wamefurahishwa na mafunzo wanayopata kwani utendaji wa kazi utakuwa wa ufanisi mkubwa.
@ortamisemi
@mtwarars_habari
@msemajimkuuwaserikali
@dc_newala
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa