• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Newala District Council
Newala District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Newala

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ujenzi
      • Planning, Statistics and Coordination
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • KIlimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • ICT & Public Relations
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Usambazaji
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
      • TASAF
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba

Walimu Newala watakiwa kutimiza wajibu wao ili ndoto walizonazo wanafunzi zifikiwe

Posted on: June 4th, 2019

Walimu wa shule za msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Newala leo Jumanne tarehe 04 Juni 2019 wametakiwa kutimiza wajibu wao ili kuwasaidia wanafunzi wanaowategemea kutimiza ndoto walizonazo.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Mussa Chimae wakati wa kikao kazi na walimu hao kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Mussa Chimae (aliyesimama) akisisitiza jambo wakati wa kikao kazi na walimu wa shule za msingi za Halmashauri ya Wilaya ya Newala.

Akizungumza kwenye kikao kazi hicho Bw. Chimae amewakumbusha walimu umuhimu na thamani yao katika maendeleo ya Halmashauri ya Wilaya ya Newala na nchi kwa ujumla. Amewataka walimu wafanye kazi kwa bidii ili ndoto za wanafunzi wanaowafundisha ziweze kutimia.

Kikao hicho kilihusisha kukumbushana maswala mbalimbali ya kiutumishi yakiwemo utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya walimu katika maeneo yao ya kazi, upandishwaji wa madaraja kwa walimu, madai ya walimu, nidhamu pamoja na mishahara.

Wakiendelea na kikao hicho walimu walipata nafasi ya kutoa hoja mbalimbali walizonazo zikiwemo madai ya mishahara kwa walimu (arreas), upandishwaji wa madaraja kwa walimu waliojiriwa mwaka 2014, malipo ya uhamisho kwa walimu, kushuka kwa nidhamu ya wanafunzi kwenye baadhi ya shule za msingi na mchango wa mwajiri kwa walimu wanaotaka kujiendeleza kimasomo.

Afisa utumishi na utawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Famili Mshaghila akitolea ufafanuzi baadhi ya hoja za walimu kwenye kikao kazi cha walimu kilichoitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala

Hoja hizo zilisikilizwa na kutolewa ufafanuzi na Afisa Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Famili Mshaghira na Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Ibrahim Mwakibete ambapo walimu walielezwa kuwa madai yao kama yalivyowasilishwa yamepokelewa na yanafanyiwa kazi, watumishi wanaotakiwa kupandishwa madaraja kwa sasa ni wale waliopo kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2017-2018 na waliotimiza miaka mitano kazini mpaka kufikia tarehe 30 June 2018 tangu kuajiriwa kwao.

Walimu wa shule ya msingi za Halmashauri ya Wilaya ya Newala wakisikiliza kwa makini kwenye kikao kazi kilichoitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala.

Aidha Bw. Chimae pia amewataka watumishi kukaa kwenye vituo vyao vya kazi na wanapotaka kusafiri au wakiwa na udhuru wawe na ushahidi wa ruhusa zao kwa maandishi. Pia amewataka Waratibu Elimu Kata na Walimu Wakuu kuchukua hatua  za kinidhamu pale inapobidi ili kuepuka mmomonyoko wa maadili katika maeneo yao ya kazi.

Kikao kazi hicho ni kikao cha kawaida ambacho Mkurugenzi Mtendaji hufanya na watumishi wake kwa makundi mbalimbali ambapo leo alifanya na walimu wote wa shule za msingi na kikao hicho kilihudhuriwa na Afisa Utumishi na Utawala, Afisa Elimu Msingi, Maafisa Elimu Kata, Walimu wakuu na walimu wote wa kawaida wa shule za msingi zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Newala.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -HALMASHAURI YA WILAYA YA NEWALA December 29, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILII WA MAHOJIANO January 06, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2021 MNYAMBE SEKONDARI July 10, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 22, 2022
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • RAIS SAMIA AMEBORESHA SEKTA YA ELIMU NEWALA DC

    March 25, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA KINYWA NA MENO WAHUDUMIA WAGONJWA 319 NEWALA DC

    March 24, 2025
  • MIAKA 4 YA RAIS DKT. SAMIA SALUHU HASSAN AMEBORESHA HUDUMA ZA AFYA

    March 19, 2025
  • NEWALA DC YANUFAIKA NA JENGO LA UTAWALA,WATUMISHI

    March 18, 2025
  • Ona Zote

Video

Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Historia ya Halmashauri
  • Idara ya Rasilimali Watu

Kurasa mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Poralg
  • Secretariet ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Newala

    Anuani ya Posta: P.O. Box 16

    Simu: +255232410251

    Mobile:

    Barua pepe: ded@newaladc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma zetu

Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa