NEWALA, MTWARA
Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Kanali Patrick Sawala ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Newala kwa kupata hati safi kutokana na Usimamizi nzuri wa mapato na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kufuata miongozo ya Serikali katika kuwahudumia wananchi.
Mhe Sawala ametoa pongezi hiyo Juni 27,2024 wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kupokea na kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kitangari.
" Niendelee kutoa hongera kwa kutekeleza maagizo ya Serikali na miongozo ambayo inasema Halmashauri zetu zinatakiwa kutenga asilimia 40 kwa ajili ya Vijana,wanawake na watu wenye mahitaji maalum na kweli nimeona kwenye taarifa ya makusanyo yenu ya ndani mmetenga shilingi Milioni 85 kwa ajili ya makundi hayo lakini pia nimeona mmetenga shilingi Milioni 255 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na fedha zimepelekwa kwenye miradi Hongereni sana " amesema Kanali Sawala .
Aidha amewaomba Madiwani kuhakikisha miradi yote inasimamiwa na kukamilika kwa wakati huku akiitaka Halmashauri kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kuwahudumia wananchi ili wapate huduma Bora.
Kwa upande wake Kaimu Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) Ndugu Geofrey Mwamba ambaye alisoma taarifa ya ukaguzi amesema kwa miaka 3 kuanzia 2020/2021,2021/2022, 2022/2023 Halmashauri ya Wilaya ya Newala ilikarikadiria kukusanya mapato zaidi ya Bilioni 5.254 kutoka vyanzo vya ndani vya mapato ambapo ilifanikiwa kukusanya zaidi ya Bilioni 4.282 sawa na asilimia 76 ya bajeti.
Ndugu Mwamba ameipongeza Halmashauri kwa kutekeleza vizuri bajeti yake hadi kufanikiwa kupata hati safi kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ikiwa ni mara 4 mfulurizo.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa