NEWALA MTWARA
Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Rajabu Kundya amewaasa watendaji kata wa Newala DC kuchagua viongozi Bora katika uchaguzi wa serikali za mitaa,ambao watakuwa mstari wa mbele katika kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa Afua bora za lishe katika Jamii.
Mhe. Kundya amesema hayo jana Novemba 14,2024 katika kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa Afua za lishe robo ya kwanza 2024/25 kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri na kuhudhuriwa na wajumbe wakiwemo wakuu wa idara na vitengo,Mkurugenzi mtendaji ,watendaji kata,Wasimamizi wa shughuli za Afya na Viongozi wa Serikali.
" Upo uhusiano baina ya kura na lishe, maana mpango wetu wa utekelezaji wa Afua za lishe unategemea na ufanisi wa viongozo watakaochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa 27 Novemba 2024"
"Wao ndio watawakabili wananchi kwa hili na lile ili wachangie chakula na kuleta mafanikio katika suala la lishe,hivyo kama tukifanya makosa kwenye uchaguzi huu tukapata viongozi wa hovyo,basi mtaona mambo yetu yataendela kukwama zaidi na kutuingiza katika janga la watoto wetu kupata udumavu na athari nyingine zitokanazo na Lishe" amesema Kundya.
Aidha taarifa ya tathmini iliyowasilishwa na Afisa Lishe Halmashauri ya wilaya ya Newala, Bi. Jane Mgaza,imebainisha mafanikio ya hali ya lishe ambapo katika ipimaji wa Kadi ya alama ya kijani, kata nyingi zimetekeleza Afua za Lishe kuanzia asilimia 80-100.
Mhe Kundya amepongeza mafanikio hayo na kuendelea kutoa msisitizo kwa timu ya Lishe kwenda kuhamasisha Jamii kuchangia chakula shuleni ili watoto wote wapate chakula wakiwa shuleni na pia ameelekeza watendaji kata ambao kata zao hazijafanya vizuri katika utekelezaji wa afua za lishe kwenda kuhamasisha zaidi wananchi kuzingatia ulaji wa lishe Bora .
Kupitia taarifa ya Tathmini ya utekelezaji wa shughuli za Afua za lishe robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/25,Kitengo cha Afya na Lishe kimefanikiwa kutembelea na kutoa Elimu ya Lishe vijiji 30 katika maadhimisho ya siku ya Lishe na Afya ya Kijiji (SALIKI), kutoa mafunzo ya Lishe kwa watendaji 22 na maafisa Tarafa 4 na watoa huduma za lishe katika vituo vyote vya kutolea huduma .
@ortamisemi
@mtwarars_habari
@dc_newal
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa