WAANDIKISHAJI WASAIDIZI NA WAENDESHAJI WA VIFAA VYA BVR ngazi ya kata,Jimbo la Newala Vijinini wametakiwa kuzingatia maelekezo,kanuni na miongozo ya Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi Pamoja na kutumia elimu na ujuzi waliopata katika kutekeleza kwa nadharia na vitendo zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura ambalo litaanza Januari 28, 2025 na kumalizika Februari 3,2025
Hayo yamesemwa Jana na Afisa Mwandikishaji Msaidizi Jimbo la Newala Vijini Ndugu Mohamedi Muhidini wakaki akifunga mafunzo ya siku mbili kwa waandikishaji wasaidizi na waendeshaji wa vifaa vya BVR yaliyofanyika kuanzia 25-26 Januari katika ukumbi wa Chuo cha Ualimu kitangari .
" Napenda mutumie muda wenu wa ziada kusoma na kupitia maelekezo yote mliyopewa ili kuongeza uelewa zaidi kuhusu wajibu na majukumu yenu katika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura kwa usahihi na ufanisi mkubwa"
Aidha Muhidini amewasitiza kuzingatia kwa umakini utunzaji wa vifaa vya uandikishaji kwa kuwa vifaa hivyo vimenunuliwa kwa gharama kubwa na vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya uandikishaji nchini.
Katika Jimbo la Newala Vijijini jumla ya waandikishaji wasaidizi na waendeshaji wa vifaa vya BVR 390 wameajiriwa kwa ajili ya kufanya kazi ya uandikishaji wa wapiga kura katika vituo 151 vilivyotengwa kufanyika zoezi la uboreshaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura.
@ortamisemi
@msemajimkuuwaserikali
@mtwarars_habari
@tumeyauchaguzi_tanzania
@dc_newala
@newalafmtz
@samia_suluhu_hassan
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa