Korosho ni zao kuu la biashara kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara ikiwemo Wilaya ya Newala. Zao hili ni moja ya mazao yanayoiingizia Halmashauri ya Wilaya ya Newala mapato na kuiwezesha kuendesha shughuli zake za kuleta maendeleo kwa wananchi wa Newala. Akizungumza na wananchi kupitia mkutano wa baraza la madiwani, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Mussa Chimae, alieleza kuwa kwa msimu huu wa korosho pembejeo zilizotengwa kwa ajili ya wakulima ni tani 1013.647 za salfa ya unga na dawa za maji lita 18584. Hata hivyo hadi kufikia tarehe 29/09/2017 jumla ya tani 920.817 za salfa ya unga na lita 18541 za dawa ya maji zimeweza kupokelewa na kusambazwa kwa wakulima. Na pembejeo ambazo hazijapokelewa hadi sasa ni tani 92.83 za salfa ya unga na lita 43 za dawa ya maji.
Pia alieleza kuwa mavuno na mauzo ya korosho kwa wakulima yameshaanza na hadi kufikia tarehe 30/10/2017 jumla ya kilo 2,103,940 zimeuzwa kupitia minada miwili ambapo mnada wa kwanza jumla ya kilo 403,247 zimeuzwa na Halmashauri kukusanya jumla ya Tsh. 17,541,244.50.
Hata hivyo Bw. Chimae ameeleza changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwa wakati huu zikiwemo ucheleweshaji wa pembejeo kutoka bodi ya korosho, kwani pembejeo kwa msimu huu zilianza kuletwa mwezi wa saba na zilizoletwa ni chache ukilinganisha na mahitaji halisi ambayo ni tani 1125 za salfa ya unga na lita 1o1250 za dawa za maji.
Pia Bw. Chimae amewataka wakulima kufungua akaunti benki kwa kuwa malipo ya kipindi hiki yanapitia benki na mkulima hapewi pesa mkononi.
Msimu wa ununuzi wa korosho ghafi za wakulima nchini Tanzania kwa mwaka 2017/2018 ulifunguliwa rasmivkitaifa tarehe 01/10/2017.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa