Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo, leo tarehe 17/10/2019 amefungua rasmi kampeni ya kitaifa ya kutoa chanjo ya Surua Rubella na Polio kwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Uzinduzi huo umefanyika katika kituo cha afya cha Kitangari ambapo wazazi wamehimizwa kuzingatia maelekezo na kuwapeleka watotokupata chanjo pale wanapohitajika.
Lengo la kampeni hii ni kuzuia na kupambana na magonjwa yanayozuilika kwa watoto wenye umri kati ya miezi 9 hadi miaka 4 namiezi 11.
Aidha chanjo hii inaongeza kinga kwa watoto hivyo wanatakiwa kupelekwa kwenye maeneo ambayo zinatolewa ili wazipate tena hata kama wameshapata chanjo hizo katika utaratibu wa kawaida wa kutoa huduma za chanjo.
Kampeni hii itafanyika kwa siku 5 kuanzia tarehe 17 hadi 21/10/2019 na jumla ya watoto 14,308 wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya Surua Rubella na watoto 9,196 wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya Polio ya sindano kwa Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa