Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Newala leo tarehe 07/02/2020 limepitisha makadirio ya bajeti ya shilingi 16,733,517,054 kwa ajili ya kugharamia matumizi mbalimbali ya Halmashauri na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2020/2021.
Makadirio ya bajeti hiyo yanahusishaTsh. 12,392,373,000 kwa ajili ya mishahara toka Serikali kuu; Tsh. 10,548,000 kwa ajili ya mishahara itokanayo na mapato ya ndani ya Halmashauri; Tsh. 1,510,409,000 kwa matumizi ya kawaida na Tsh. 2,820,187,054 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Aidha, wajumbe wa baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Newala baada ya kupokea uwasilishaji wa makadirio hayo ya bajeti walishauri kuwa ukusanyaji wa mapato ya ndani uongezeke ili kuwezesha kupeleka fedha nyingi zaidi katika miradi ya maendeleo hasa miradi ambayo haikukamilika katika miaka iliyopita.
Wakati huohuo baraza hilo la madiwani limewapongeza walimu wakuu wa shule za msingi waliofanya vizuri katika usimamizi wa miradi iliyopata pesa za malaria bas malipo kulingana na matokeo (P4R) kwa kuwapatia vyeti maalum vya pongezi ambavyo vilitolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Newala Bw. Daniel Zenda ambaye alihudhuria kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo.
Shule zilizopata pongezi hizo ni shule ya msingi Mnyeu ; shule ya msingi Mnyengachi na shule ya msingi Chilangala.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa