Halmashauri ya Wilaya ya Newala imeadhimisha kilele cha wiki ya mazingira tarehe 09 Juni 2017 katika kijiji cha Chikalule wilayani Newala.
Mkuu wa Wilaya ya Newala Bi. Aziza Mangosongo (aliyekaa katikati) akizungumza jambo na mwenyekiti wa kijiji cha Chikalule (wa kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Mussa Chimae
Katika maadhimisho hayo ambayo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa Wilaya ya Newala Bi. Aziza Mangosongo, mambo mengi yalifanyika yakiwemo upandaji wa miti, utoaji wa vyeti kwa kata zilizoshinda katika mashindano ya usafi wa mazingira na uchangiaji wa damu salama.
Mkuu wa Wilaya ya Newala Bi. Aziza Mangosongo akishiriki katika zoezi la kupanda miti katika kijiji cha Chikalule wilayani Newala
Maadhimisho hayo pia yalihudhuriwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Mussa Chimae, makamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Mhe. Swalehe Fakihi, mwenyekiti wa kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira Mhe., Diwani wa Kata ya Mkoma II Mhe., kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Newala, wakuu wa Idara na Vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala na wananchi wa kijiji cha Chikalule na vijiji jirani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala akizungumza na washiriki wa kilele cha wiki ya mazingira kilichofanyika katika kijiji cha Chikalule wilaya ya Newala.
Akizungumza na washiriki wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya mazingira Mhe. Mangosongo aliwahimiza kutunza mazingira ili nayo yawatunze kwa kupanda miti kwenye maeneo ya shule, ofisi, maeneo ya wazi, mashamba na vyanzo vya maji.
Kauli mbiu ya mazingira ya kitaifa kwa mwaka huu ni “Hifadhi mazingira kwa Tanzania ya viwanda”
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa