NEWALA
Viongozi wapya 2675 wa Serikali za vijiji na Vitongoji walioshinda kwenye nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024 wamekula kiapo cha uadilifu jana kwa ajili ya kuanza kazi ya kuwatumikia wananchi katika masuala mbalimbali ya maendeleo.
Viongozi hao ambao wote kutoka chama cha mapinduzi (CCM) wamekula kiapo katika Makao makuu ya Halmashauri mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Halmashauri ya Mji Newala Bi Elicy Mkonya, ambaye amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa uadilifu kwa maslahi ya watu wote katika vijiji au vitongoji.
Aidha kwa mujibu wa Taarifa ya Afisa Uchaguzi aliyotoa akiwa Ofisini kwake kwa niaba ya Msimamizi wa Uchaguzi imesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) Newala DC kimeshinda kwa asilimia 100 katika uchaguzi huo ambapo wagombea 2675 wa CCM wamechaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwemo Uenyekiti wa Kijiji nafasi 107,Uenyekiti wa Vitongoji nafasi 302,wajumbe mchanganyiko nafasi 1410 na wajumbe wanawake nafasi 856 .
Katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka huu Newala DC , vyamba 5 vya siasa vilijitokeza kushiriki kikiwemo chama cha CCM,ACT WAZALENDO,CUF ,NCCR MAGEUZI NA CHADEMA .
@ortamisemi
@msemajimkuuwaserikali
@mtwarars_habari
@dc_newal
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa