Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala leo tarehe 10/07/2020 wameshiriki kwenye bonanza la kujenga umoja wao lililowashirikisha watendaji wa kata pamoja na watumishi wa makao makuu ya Halmashauri hiyo.
Timu ya mpira wa miguu ya watendaji wa kata iliyoshiriki kwenye bonanza la leo.
Bonanza hilo lilihusisha michezo ya aina tatu ikiwemo mchezo wa mpira wa mikono "Volleyball", netiboli na mpira wa miguu.
Matokeo ya michezo hiyo ni kuwa kwenye mchezo wa mpira wa mikono watumishi wa makao makuu ya Halmashauri waliibuka washindi kwa kushinda seti zote tatu; mchezo wa netiboli timu zote mbili zilitoka sare na mchezo wa mpira wa miguu timu ya makao makuu ya Halmashauri iliibuka mshindi kwa kufunga magoli manne kwa mawili.
Wachezaji wa mpira wa miguu wa timu ya makao makuu ya Halmashauri wakifurahi kukabidhiwa zawadi ya mbuzi baada ya kuibuka washindi wa mpira wa miguu.
Timu ya mpira wa miguu ya makao makuu ya Halmashauri walipatiwa zawadi ya mbuzi kwa kuibuka washindi na timu ya watendaji wa kata ya netiboli walipatiwa zawadi ya kuku.
Mgeni rasmi katika bonanza la leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Bw. Famili Mshaghila akizungumza na wachezaji wa timu zote mbili za netiboli kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Mgeni rasmi katika bonanza hilo ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Famili Mshaghila ambaye alifungua michezo hiyo na kukabidhi zawadi kwa washindi.
Kikosi cha timu ya mpira wa miguu ya watumishi wa makao makuu ya Halmashauri kilichoshiriki kwenye bonanza la leo.
Bonanza hili ni muendelezo wa michezo ya mara kwa mara ya watumishi inayolenga kujenga umoja na ushirikiano wa watumishi na kuchangamsha mwili na akili hivyo kuongeza morali ya ufanyaji wa kazi.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa