Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala leo Alhamisi tarehe 26/03/2020 wamepatiwa mafunzo elekezi ya ujazaji wa mfumo wa wazi wa mapitio na tathmini ya utendaji kazi (OPRAS) kwa menejimenti na watumishi yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha walimu Kitangari.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala wakisikiliza kwa makini mafunzo elekezi ya OPRAS
Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uelewa watumishi juu ya maana ya mfumo wa OPRAS, mpango kazi wa OPRAS wa mwaka, ujazaji wa OPRAS, Majukumu ya wahusika katika mfumo wa OPRAS na matumizi yake.
Mfumo huo wa OPRAS ni muhimu kwa kuwa unatumika kupima uwajibikaji na utendaji wa mtumishi unaohusu majadiliano kati ya mtumishi na msimamizi wake.
Mafunzo hayo yametolewa na Idara ya Utumishi na Utawala kwa wakuu wa idara na vitengo ili kuhakikisha kunakuwa na ufanisi katika upimaji wa utekelezaji wa majukumu wakati wa kutoa huduma kwa jamii na yalifunguliwa rasmi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bi. Magreth Likonda.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa