Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Newala vijijini Bw. Duncan Thebas leo siku ya Ijumaa tarehe 07/08/2020 amefungua mafunzo ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha ualimu Kitangari.
Akifunga mafunzo hayo Bw. Thebas, alianza kwa kuwapongeza washiriki hao kwa kuteuliwa kuwa Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata.
"Tume imewateua ninyi kwa mujibu wa sheria na kwa kuzingatia utendaji na uzoefu wenu katika masuala ya uchaguzi ". Alisema Bw. Thebas
Wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kata wakifuatilia mafunzo yanayotolewa katika mafunzo yaliyotolewa leo kwenye ukumbi wa mikutano wa chuo cha walimu Kitangari.
Wasimamizi hao wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata kwa jimbo la Newala vijijini wametakiwa kuzingatia wajibu na majukumu yao wanayoelekezwa kwenye mafunzo hayo ili kufanikisha zoezi la uchaguzi mkuu wa Rais na wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na madiwani wa Tanzania Bara.
"Pamoja na baadhi yenu kuwa wazoefu katika kuendesha uchaguzi, mhakikishe mnazingatia maelekezo mtakayopewa na Tume badala ya kufanya kazi kwa mazoea. Lakini pia, hakikisheni mnazingatia matakwa ya Katiba, sheria na kanuni zinazosimamia zoezi la uchaguzi. Alisisitiza Bw. Duncan
Washiriki hao wa mafunzo pia wametakiwa kuvishirikisha vyama vya siasa na wadau wengine wa uchaguzi katika masuala ambayo wanastahili kushirikishwa.
Mafunzo hayo yatafanyika kwa siku tatu kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata 44 wa jimbo la Newala vijijini kuanzia leo tarehe 07/08/2020 mpaka tarehe 09/08/2020 katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha ualimu Kitangari.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa