Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na waandikishaji wa wapiga kura wametakiwa kufuata kanuni zinazowaongoza ili kufanikisha majukumu yao.
Hayo yamesemwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo wakati akifungua mafunzo ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na waandikishaji wa wapiga kura wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala siku ya Jumamosi tarehe 05/10/2019.
Mkuu wa Wilaya ya Newala, Mhe. Aziza Mangosongo akizungumza wakati akifungua mafunzo ya wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na waandikishaji wa wapiga kura.
Akifungua mafunzo hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Mhe. Mangosongo amewaeleza wasimamizi na waandikishaji hao kuwa, Serikali imewaamini na kuwapa dhamana hiyo, hivyo wafuate kanuni zinazowaongoza ili kutoiingiza hasara Serikali.
"Uteuzi wenu umezingatia kanuni za Serikali za mitaa kifungu namba 7(1) na kifungu namba 10(2), ninawaasa kuwa mkafanye kazi hii kwa uaminifu mkubwa, mkizingatia kanuni zinazowaongoza katika kufanya kazi hiyo" alisema Mhe. Mangosongo.
Mafunzo hayo yameambatana na kuapishwa kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi 129 na waandikishaji wa wapiga kura 302 walioweka kiapo chao mbele ya Mhe. Hakimu Mkazi Glory Mwakihaba.
Wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi na waandikishaji wa wapiga kura wakiapa kiapo cha uaminifu katika kutekeleza majukumu yao.
Uandikishaji wa wapiga kura unatarajiwa kufanyika kwa siku saba kuanzia Jumanne tarehe 08 hadi tarehe 14/10/2019 katika vitongoji vyote 302 vya Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa