Jana Ijumaa tarehe 30/04/2021 imefanyika tafrija fupi ya kuwaasa na kuwaombea watahiniwa wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Mnyambe wanaotarajiwa kuanza kufanya mtihani wa Taifa kuanzia Jumatatu tarehe 03/05/2021 na kumaliza tarehe 17/03/2021.
Watahiniwa wa kidato cha sita katika shule ya sekondari Mnyambe wakisikiliza nasaha wanazopewa ikiwa ni maandalizi ya kuelekea kufanya mitihani ya kuhitimu kidato cha sita inayotarajiwa kuanza Jumatatu tarehe 03/05/2021
Shule ya Sekondari Mnyambe ina watahiniwa wa kidato cha sita 32 wanaochukua fani za sayansi kwa michepuo ya CBG (Kemia, Baiolojia na Jiografia) wanafunzi 28 na PCB (Fizikia, Kemia na Bailojia) wanafunzi 4.
Tafrija hiyo ilihudhuliwa na wanafunzi wa kidato cha sita wa shule hiyo ya Sekondari Mnyambe, walimu wao, viongozi wa dini na Serikali, mgeni rasmi akiwa Bw. Friday Sondasy, Afisa Elimu Sekondari, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Bw. Duncan Thebas.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa