NEWALA, MTWARA
SERIKALI ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, imetoa shilingi Milioni 320 kwa mwaka wa fedha 2023/24, kwa ajili ya Mradi wa Ujenzi wa nyumba 4 za Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Mradi huo unatekelezwa kwa lengo la kuwaondolea adha ya makazi Watumishi wa Umma ambapo kwa mwaka fedha 2021/22 Halmashauri imejenga nyumba 3 zenye thamani ya shilingi Milioni 240 hivyo kufanya nyumba zitakazojengwa kuwa Saba.
Leo mapema asubuhi Kitengo cha Habari na Mawasiliano kimezungumza na Fundi Ujenzi wa mradi huo Ndugu Hamisi Bakari Nahoda ambaye amesema ujenzi unaendelea vizuri kwa sababu Mzabuni anapeleka malighafi za ujenzi kwa wakati.
Amesema mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miezi 3 kuanzia Juni 2024 na utamalizika Septemba 2024 .
Aidha Nahoda ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuleta miradi na kuanzisha mfumo wa NeST ambao umesaidia kuleta uwazi na kuondoa malalamiko kwa wazabuni na Mafundi wanaoomba kujenga miradi ya serikali.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa