UJUMBE WA SHUKRANI KWA MHESHIMIWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan
Uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala unatoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutupatia fedha milioni 464 kwa ajili ya Ujenzi wa miundombinu ya Kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari Nanda.
Kupitia uongozi wake madhubuti na wenye maono, sasa wanafunzi wa Wilaya ya Newala watapata fursa ya kuendelea na elimu ya juu ya sekondari wakiwa katika mazingira bora na rafiki kwa ujifunzaji. Hatua hii si tu kwamba inaongeza fursa za kielimu, bali pia inachochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wananchi wetu.
Tunamuombea Mheshimiwa Rais afya njema, maisha marefu na uongozi wenye mafanikio zaidi kwa taifa letu.
Asante sana Mama Samia kwa kutujali, kutusikia na kutuchukulia kama sehemu ya vipaumbele vya maendeleo ya nchi hii.
Elimu Bora ni Msingi wa Taifa Imara!
Kitangari,Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa