Halmashauri ya wilaya ya Newala imetoa Mafunzo kwa wanufaika wa mikopo ya asilimia kumi ya mapato ya ndani yaliyotolewa kupitia Idara ya maendeleo Jamii ili kuhakikisha mikopo hiyo inatumika vyema kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Halmashauri Desemba 20,2024 yakisimamiwa na Maafisa Maendeleo Jamii ambao ni wadau muhimu katika usimamizi wa mikopo .
Maafisa hao akiwemo Mkuu wa Division ya maendeleo Jamii Ndugu Geofrey Chitanda wametoa maelekezo kwa wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu kuhakikisha mikopo hiyo inatumika kwa malengo yalikusudiwa ambayo ni kukuza ujasiriamali, kuboresha kipato, na kuinua hali ya maisha ya wanawake, vijana, na watu wenye ulemavu.Piamwanasheria wa Halmashauri Ndugu Shafii Mtinia ametoa rai kuhusu kanuni na taratibu za mikopo hiyo Kwa kuzingatia sheria zinazohusiana na utoaji wa mikopo ya asilimia kumi, na namna ya kutatua migogoro inayoweza kutokea katika kikundi husika
Kwa upande wa wanufaika wameishukuru serikali awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuwajali wajasiriamali kuwapatia mikopo na kuaahidi kuifanyia kazi ipasavyo ili kujikwamua kiuchumi
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa