Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, Ndugu Duncan Thebas, ametoa pongezi kwa Waheshimiwa Madiwani akiwatambua kwa kazi kubwa waliyoifanya katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wao.
"Ninatoa pongezi za dhati kwa Waheshimiwa Madiwani kwa ushirikiano mkubwa mlioonesha katika kipindi chote cha miaka mitano. Mmefanya kazi kwa bidii, kwa moyo wa kizalendo na kwa malengo ya kuleta mabadiliko chanya kwa wananchi wa Halmashauri ya Newala. Ushirikiano wenu na watendaji wa Halmashauri umeiwezesha Newala kusonga mbele katika nyanja mbalimbali za maendeleo."
"Kupitia uongozi wenu, tumeimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani, kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kama elimu, afya na maji, pamoja na kuimarisha misingi ya utawala bora. Mchango wenu hautafutika na utaendelea kuhifadhiwa katika historia ya maendeleo ya Halmashauri yetu. Nawashukuru kwa dhamira, weledi na mshikamano mliouonesha."
Kauli hiyo aliitoa wakati wa mkutano maalum wa kuvunja Baraza la Madiwani uliofanyika Juni 20, 2025 katika ukumbi wa Halmashauri ya Newala.
Kitangari,Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa