Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Mhe. Mfaume Tamimu Ladda leo tarehe 15/02/2021 amekabidhi viti na meza 500 kwa ajili ya matumizi ya wanafunzi wa shule za Sekondari Mpotola, Mnyambe, Lengo, Makukwe, Maputi na Mtopwa.
Akikabidhi viti na meza kwa shule hizo sita, Mhe. Ladda amewataka walimu na wanafunzi kutunza viti na meza hizo na kuhakikisha haviharibiki.
Makabidhiano hayo yamehusisha Lengo sekondari viti na meza 100; Makukwe sekondari viti 120 na meza 100; Maputi sekondari viti 40 na meza 60; Mnyambe sekondari viti na meza 80; Mpotola sekondari viti na meza 100; na Mtopwa sekondari viti na meza 60.
Hii ni awamu ya kwanza ya mgao wa viti na meza kwa shule hizo sita, na awamu ya pili itahusisha ugawaji wa viti na meza 150 kwa shule za Sekondari Chihangu, Malatu, Mkoma, Mpelepele na Vihokoli.
Makabidhiano hayo kwa wakuu wa shule zote sita yamefanyika katika shule ya sekondari Mpotola ikiwa ni jitihada za Halmashauri ya Wilaya ya Newala kupitia fedha za mfuko wa elimu ili kudhibiti upungufu wa viti na meza kwa baadhi ya shule za sekondari zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa