Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe.Alhaji Mwangi Rajab Kundya,Kamati yake ya Ulinzi na Usalama na Wananchi wakiwa tayari kwa ajili ya kupokea Mwenge wa Uhuru maalum kwa Mwaka 2021 katika Eneo la Shule ya Msingi Makukwe II ukitokea Wilayani Tandahimba,jumla ya Miradi saba(07) inayotarajiwa kupitiwa na Mbio za Mwenge ambayo ni ufunguzi wa Madarasa mawili(02) na Ofisi Moja(01) ya Shule ya Sekondari Makukwe,pia Kiongozi wa Mbio za Mwenge atazindua Klabu ya wapinga Rushwa Shuleni hapo.Kiongozi wa mbio za Mwenge atagawa Pikipiki kumi na tano (15) kwa vikundi viwili vya Bodaboda na Bajaji moja (01) kwa kikundi cha Walemavu,pia na kuona /kukagua shughuli za Wajasiliamali,Wanawake na wenye Ulemavu katika eneo la Shule ya Sekondari Ushirika .
Ujenzi wa Barabara ya Kiduni kuelekea Makondeko yenye urefu wa 1KM yenye kiwango cha Lami itawekewa jiwa la Msingi na kisha kuelekea katika Mradi wa Maji Chitandi kuona na kukagua maendeleo ya ujenzi baada ya hapo Mwenge utaelekea Tupendane ambao utazindua kiwanda cha kukoboa na kusaga Nafaka cha HKM na baada ya hapo utaelekea Zahanati ya Tupendane ambapo utajioonea/ kukagua na kupata taarifa ya Mifumo ya TEHAMA,uzinduzi wa Zahanati ya Tupendane na Kupata taarifa ya wilaya ya Lishe na kukagua Banda la kutoa Elimu ya Lishe.
Mwenge wa Uhuru Maalum utahitimisha mbio zake katika wilaya ya Newala katika Eneo la Mkesha Stendi ya Mabasi Luchingu ambapo kiongozi wa mbio za Mwenge atajionea na kukagua juhudi za Wilaya katika kutoa Elimu ya TEHAMA,LISHE,kupambana na Malaria,UKIMWI,Madawa ya Kulevya na Rushwa.Pia Wananchi watapata fursa ya kusikiliza Risala ya Utii,Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru Maalum na kupata burudani.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa