DARESSALAAM,
Maafisa Habari Nchini wametakiwa kuhamasisha na kusambaza habari zitakazowezesha kufanikiwa kwa zoezi la Daftari la kudumu la wapiga kura.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Habari na Elimu ya mpiga kura Bi Giveness Aswile wakati akiwasilisha mada katika mkutano wa Tume na Maafisa Habari kuhusu Uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura mwaka 2024,uliofanyika katika Ukumbi wa mlimani city Jijini Daressalaam.
"Tunawaomba na kuwasihi, kutumia nafasi na fursa mlizonazo kuhakikisha kunakuwepo na taarifa za mara kwa mara za kuelezea kinachoendelea kwenye zoezi hili kwenye maeneo yenu"
" Tumieni mbinu na uwezo wenu wote kuhakikisha mnahamasisha wananchi kujitokeza kuandikishwa kuwa wapiga Kura" amesema Bi Giveness
Aidha Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania imekamilisha maandalizi ya vituo vya kuandikisha wapiga Kura ambapo vituo 40,126 vitatumika katika Uboreshaji wa Daftari la wapiga Kura 2024 kati ya hivyo,
Vituo 39,709 vipo Tanzania Bara na 417 Vipo Zanzibar.
Bi Giveness amesema idadi hiyo ni ongezeko la vituo 2,312 ikilinganishwa na vituo 37,814 vilivyotumika 2019/2020.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa