Maadhimisho ya siku ya motto Afrika wilayani Newala
Tar 20 Juni 2017 yalifanyika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika wilayani Newala katika kijiji cha Nangudyane.Maadhimisho hayo yaliendena na kauli mbiu isemayo “Maendeleo endelevu 2030 imarisha ulinzi na fursa sawa kwa watoto”.
Maandamano ya watoto
Mgeni Rasmi akipokewa kwa maandamano ya watoto
Maadhimisho hayo yalihudhuliwa na Mh. Mkuu wa wilaya Newala akiwa mgeni rasmi.
Katika maadhimisho hayo kulitolewa elimu na nasaha mbali mbali juu ya ulinzi na afya kwa motto kupitia nyimbo,maigizo na risala.
Pia risala ya watoto ilisomwa na mkuu wa shule ya msingi Tumaini ikielezea changamoto mbali mbali kwa watoto hasa katika shule ya msingi Tumaini,ikiwa ni pamoja na upungufu wa madarasa,upungufu wa matundu ya choo,walimu na nyumba za walimu.
Mkuu huyo alimuomba mgeni rasmi kujionea hali halisi ya Nyumba ya Mkuu wa shule na choo chake na vyoo vya wanafunzi ambavyo haviko katika hali nzuri.
Afisa maendeleo ya jamii ambaye alimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halimashauri ya wilaya Newala Bi.Christina Kambuga alitolea majibu na ufafanuzi juu ya mipango na mikakati ya serikali katika kumlinda mtoto na mipango ya maendeleo katika kijiji hicho na Nangudyane .
Mkuu wa wilaya Newala ambaye pia alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo aliongea na hadhira juu ya ulinzi na usalama kwa watoto na jukumu la wazazi,walezi na jamii kwa ujumla katika kumlinda na kumthmin mtoto.
Pia mkuu wa wilaya alifanya uzinduzi wa chanjo kwa watoto na kutembelea nyumba na choo cha mwalimu mkuu pamoja na vyoo vya wanafunzi.
Aidha mgeni rasmi alitoa zawadi kwa makundi yaliyotumbuiza na kwa watoto wote waliofika katika maadhimisho hayo.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa