Mwenge wa Uhuru Maalum mwaka huu wa 2021 katika Wilaya ya Newala umekimbizwa katika Miradi saba(7) yenye jumla ya gharama kiasi cha fedha Bilioni Moja,Milioni Mia Saba na Ishirini na Mbili ,Laki Nane Kumi na Mbili Elfu Mia Saba Sitini na Tano na Senti Sabini na nne(Tsh.1,722,812,765.74) Fedha hizi zikiwa ni mchango wa serikali kuu iliyochangia kiasi cha Tsh.1,404,451,502.35 sawa na 81.52%,Michango ya Wananchi ni kiasi cha Tsh.113,007,000.00 sawa na 6.56%,Wilaya ya Newala imechangia kiasi cha Tsh.48,000,000.00 sawa na 2.79%.Fedha kutoka kwa hisani ni Tsh.157,354,263.39 sawa na 9.13%
Miradi saba iliyopitiwa na Mwenge ni Ujenzi wa Madarasa mawili na ofisi Moja katika shule ya Sekondari Makukwe yaliyogharimu kiasi cha Tsh.46,000,000.00.Ugawaji wa Pikipiki Kumi na Tano (15) na Bajaji Moja(01),mradi uliogharimu kiasi cha Tsh.44,000,000.00
Kiasi cha Tsh.927,392,502.00 kimetumika katika mradi wa ujenzi wa miundo mbinu ya Maji Chitandi ikiwa ni Fedha kutoka Serikali kuu,Serikali Kuu imechangia pia Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Kiduni kuelekea Makondeko kwa kiwango cha lami chenye urefu wa 1KM,kiasi cha Tsh.477,500,094.00
Mradi wa Ujenzi wa Zahanati ya Tupendane imefadhiliwa na Wahisani kwa kiasi cha Tsh.117,354,263.39 huku Wananchi wakichangia kiasi cha Fedha Tsh.111,007,000.00 katika mradi wa Kampuni ya HKM Super Sembe.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa