Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Mussa Chimae leo Jumatano tarehe 20/05/2020 amewaeleza wajumbe wa mkutano wa baraza la madiwani jitihada zinzofanywa na Halmashauri katika uboreshaji wa miundombinu ya sekta ya elimu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bw. Mussa Chimae (aliyesimama) akizungumza katika mkutano wa baraza la madiwani
Akizungumza katika mkutano huo, Bw. Chimae ameeleza kuwa ujenzi wa madarasa 16 kupitia fedha za malipo kulingana na matokeo (EP4R) umekamilika kwa asilimia 100 katika shule 16 za msingi na madarasa 9 yanayojengwa kupitia mfuko wa elimu ujenzi wake unaendelea katika shule 3 shikizi za Mtunguru B, Chikalule na Chikuti.
Wah. Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala wakifuatilia taarifa katika mkutano wa baraza la madiwani
Aidha, ujenzi wa madarasa 2 na ofisi katika shule za sekondari Mpotola na Makukwe umefikia katika hatua ya upauaji ambapo ujenzi huo unagharimu shilingi milioni 40 fedha zilizotolewa na mfuko wa elimu wa Wilaya.
Akiendelea kuzungumza kwenye mkutano huo, Bw. Chimae pia ameueleza mkutano huo kuwa, katika kipindi cha Januari mpaka Machi 2020, Halmashauri imeweza kutoa mikopo kwa vikundi 14 vya wanawake, vijana na walemavu yenye jumla ya shilingi milioni 51.
Mkutano huo wa baraza la madiwani ni wa kawaida wa robo ya tatu kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambao umejadili taarifa za maendeleo za Halmashauri ya Wilaya ya Newala na umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa chuo cha walimu Kitangari.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa