NEWALA, MTWARA
Halmashauri ya Wilaya ya Newala kupitia Idara ya Afya, Ustawi wa jamii na Lishe imesimamia na kutekeleza zoezi la Mwezi wa Afya na Lishe ya watoto umri wa miezi 6-59 kuanzia Juni 1,2024 ambapo watoto 14587 sawa na asilimia 95 kati ya15355 waliopo kwenye mpango wamepata nyongeza ya Vitamini A.
TAKWIMU hizo zimetolewa na Afisa Lishe Halmashauri ya wilaya ya Newala Bi. Christine Lukinisha ambaye amesema idadi hiyo imetokana na utoaji wa elimu kwa wazazi na walezi ambao wamepata uelewa na kuzingatia umuhimu wa Afya na Lishe kwa watoto wao.
Bi Christine amesema watoto waliopata Dawa za minyoo ya tumbo ni 12829 sawa na asilimia 95 kati ya 13504 wanaotarajiwa kupata dawa hizo.
Aidha utekelezaji wa Afya ya watoto na Lishe umesaidia kuimarisha Afya na kupunguza vifo vya watoto.
Zoezi hili katika Halmashauri ya Wilaya ya Newala, limeanza kufanyika kuanzia Juni 1,2024 katika vituo vya kutolea huduma za Afya na kwenye huduma jumuishi za Vikoba na litakamilika Juni 30,2024.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa