• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za watumishi |
    • Malalamiko |
Newala District Council
Newala District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Newala

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Ujenzi
      • Planning, Statistics and Coordination
      • Rasilimali watu na Utawala
      • Fedha na Biashara
      • Afya
      • KIlimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Maendeleo ya Jamii
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Usafi na Mazingira
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • ICT & Public Relations
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Manunuzi na Usambazaji
      • Sheria
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Maji
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
      • TASAF
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Madiwani
    • Orodha ya Wahe. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba

Walimu Newala watakiwa kutokufanya kazi kwa mazoea

Posted on: April 11th, 2019

Afisa elimu taaluma kutoka sekretariet ya Mkoa wa Mtwara Bw. Mahamoud Kambona, amefanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Newala siku ya Alhamisi tarehe 11 Aprili 2019 na kufanya kikao na watumishi wa idara za elimu msingi na sekondari za Wilaya ya Newala katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala.

Akizungumza na watumishi wa idara za elimu kutoka Halmashauri ya Mji na Wilaya ya Newala Bw. Kambona amewataka walimu kuacha kufanya kazi kwa mazoea ila kujituma na kushirikiana pia kuwa wabunifu na wafuatiliaji katika utendaji wao wa kazi ili kutokomeza daraja la sifuri katika matokeo ya mitihani ya kuhitimu kidato cha nne na cha sita.

Akiendelea kuzungumza kwenye kikao hicho, Bw. Kambona amewahimiza walimu hao kuwa na uadilifu na usimamizi makini katika miradi yote inayopelekwa kwenye shule zao; kuhakikisha hakuna mwanafunzi asiyejua kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK) kwa shule za msingi; kusimamia upatikanaji wa chakula shuleni kwa ajili ya wanafunzi; vitabu vilivyopelekwa kwenye shule vitumike kama inavyotakiwa; na walimu wafanye kazi kwa upendo na mshikamano pasipo kuwa na fitina baina yao.

Hii ni sehemu ya mkakati wa Sekretariet ya Mkoa wa Mtwara upande wa elimu katika kuboresha utendaji kazi wa ofisi ya elimu Mkoa wa Mtwara ambapo maafisa waliopo kwenye ofisi hiyo wamegawana Halmashauri za kuzilea kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa shughuli za elimu na kukuza ufanisi katika utendaji kazi.

Ziara ya Bw. Kambona katika Wilaya ya Newala  ilikuwa na lengo la kujitambulisha kwa watumishi wa idara za elimu zilizopo wilaya ya Newala kuwa yeye ndiye mlezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala na Halmashauri ya mji wa Newala katika maswala yote yanayohusu elimu ya msingi na sekondari.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI -HALMASHAURI YA WILAYA YA NEWALA December 29, 2023
  • KUITWA KWENYE USAILII WA MAHOJIANO January 06, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA SITA MWAKA 2021 MNYAMBE SEKONDARI July 10, 2021
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI June 22, 2022
  • Ona Zote

Habari Mpya

  • NEWALA DC YATEKELEZA MPANGO WA TASAF KWA MAFANIKIO MAKUBWA

    July 17, 2025
  • MWEZI WA AFYA NA LISHE KWA WATOTO

    July 04, 2025
  • UJUMBE WA SHUKRANI KWA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

    July 04, 2025
  • NEWALA DC YAPOKEA MITUNGI YA GESI

    June 24, 2025
  • Ona Zote

Video

Video Zaidi

Kurasa za Karibu

  • Historia ya Halmashauri
  • Idara ya Rasilimali Watu

Kurasa mashuhuri

  • Tovuti Rasmi ya Rais
  • Poralg
  • Secretariet ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana nasi

    Kitangari,Newala

    Anuani ya Posta: P.O. Box 16

    Simu: +255232410251

    Mobile:

    Barua pepe: ded@newaladc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Usiri
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma zetu

Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa