NEWALA, MTWARA
Halmashauri ya wilaya ya Newala imepokea shilingi Bilioni 1.2 kutoka Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule za msingi na Sekondari.
Taarifa ya Mapokezi ya fedha hizo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Newala Ndugu Dancun Thebas wakati wa kikao maalum cha Baraza la Madiwani cha kujadili hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kilichofanyika ukumbi wa Chuo cha Ualimu Kitangari Juni 27,2024.
Amesema kati ya fedha hizo shilingi Milioni 250.7 zitatumika kujenga madarasa ya shule za msingi na shilingi Bilioni 1.24 zitatumika kujenga madarasa ya shule za Sekondari.
Ndugu Dancun amesema Rais amesikia kilio cha wananchi wa Newala Dc kuomba kujengewa kidato cha tano na sita hivyo kati ya fedha hizo shilingi Milioni 404 zitatumika kuanzisha ujenzi wa madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari Nanda Tarafa ya Kitangari.
Kuanzishwa kwa kidato cha tano na sita katika shule hiyo kutakuwa ni mkombozi sana kielimu kwa kuwa Halmashauri ilikuwa na shule moja ya kidato cha tano na sita katika Kijiji cha Mnyambe
Mkurugenzi Thebas amewaomba Madiwani kujipanga na kushirikiana na Menejimenti kuhakikisha miradi yote inakamilika kwa wakati kwani Rais Samia ametoa maelekezo ujenzi wa madarasa ukamilike ndani ya miezi mitatu.
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa