Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Newala zahamia rasmi Kitangari leo tarehe 17/10/2019.
Hii ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Joseph Magufuli tarehe 07/10/2019 la kuzitaka Halmashauri 31 ikiwemo ya Wilaya ya Newala kuhamia kwenye maeneo yao ya utawala ndani ya siku 30 kuanzia tarehe ya siku lilipotolewa agizo. Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Newala pamoja na idara na vitengo kuanzia leo itapatikana katika eneo la Maputi karibu na shule ya msingi Kitangari Mazoezi.
Aidha ofisi ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika pamoja na ofisi za ujenzi zinapatikana katika jengo la AMCOS Kitangari, Ofisi ya Ardhi, maliasili na mazingira inapatikana katika jengo la ofisi ya Kata ya Kitangari, ofisi ya maendeleo ya jamii inapatikana katika jengo la Jaribu Saccos Kitangari, ofisi ya idara ya elimu msingi inapatikana katika jengo la cluster shule ya msingi Kitangari B na ofisi ya idara ya elimu sekondari inapatikana katika majengo ya chuo cha ualimu Kitangari.
Pia ofisi ya idara ya Afya inapatikana katika Kituo cha Afya cha Kitangari
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala Bw. Mussa Chimae akitoa maelezo kwa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ilipotembelea Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Newala.
Kamati ya ulinzi na usalama ikiongozwa na Mhe. Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo imekagua na kuridhishwa na utekelezaji huo.
#Halmashauri ya Wilaya ya Newala Tunatekeleza
Newala
Anuani ya Posta: P.O. Box 16
Simu: +255232410251
Mobile:
Barua pepe: ded@newaladc.go.tz
Hakimiliki@2016 Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Haki zote zimehifadhiwa